Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto),
akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya kuhudumia mizigo, Ndege na
abiria ya Swissport inayotoa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA), alipofanya ziara ya siku moja ya kutembelea
uwanja huo Dar es Salaam leo.
Kamanda
wa Polisi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),
Kamishna Msaidizi (SACP), Martin Otieno (kulia), akimueleza Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto),
kuhusu hali ya usalama katika uwanja huo wakati wa ziara ya waziri huyo
katika uwanja huo Dar es Salaam leo. (Katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi George Sambali,
Foku lifti likifanya kazi ya kubeba mizigo katika ghara hilo.
Kamishna
Msaidizi wa Uhamiaji, Elizabeth Lukuwi (kushoto), akutoa maelezo kwa
Waziri Mbarawa baada ya kufika eneo la ukaguzi kwa wageni.
Kamishna
Msaidizi wa Uhamiaji, Elizabeth Lukuwi, akimpigia saluti Waziri Mbarawa
baada ya kumpa maelekezo ya utendaji kazi katika kitengo cha wageni
kiwanjani hapo.
Waziri
Mbarawa akizungumza na Raia wa Kigeni aliyemuelezea kutumia muda mwingi
zaidi ya masaa mawili kwa ajili ya upimaji wa afya uwanjani hapo ambapo
Waziri huyo aliwaagiza wahusika kuhakikisha wanatumia muda mfupi kutoa
huduma kwa wageni ambao wanakuwa wamerundikana katika eneo hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa JNIA wakiwa uwanjani hapo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Swissport, Gaudence Temu (wa pili kushoto),
akimuelekeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame
Mbarawa (wa pili kulia), jinsi kampuni hiyo inavyofanyakazi na
changamoto zake. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi George Sambali. Kushoto ni Meneja
Biashara wa TAA, Efata Lyimo.
Vifufushi vikiwa kwenye ghara jipya la Swissport.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni