KOFFI OLOMIDE AKAMATWA NA POLISI JIJINI KINSHASA

Mwanamuziki maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Koffi Olomide amekamatwa na polisi Jijini Kinshasa.

Mwandishi mmoja nchini humo ametwitti picha za tukio la kukamatwa kwa Koffi Olomide na polisi.
Koffi Olomide alitimuliwa Kenya wiki iliyopita baada ya kumpiga teke dansa wake mwanamke katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.


Picha zinazomuonyesha Koffi Olomide akiwa chini ya ulinzi wa polisi Jijini Kinshasa akipelekwa kituo cha polisi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni