MKOA WA ARUSHA WANUFAIKA NA NYUMBA 20 ZA WAUGUZI


Katibu Mkuu Wizara ya Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dr.Mpoki Mwasumbi pamoja na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa Dr. Ellen Mkondya Senkoro wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa nyumba za wauguzi katika Zahati ya Mungere Wilayani Monduli.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,maendeleo ya jamii,Jinsia,wazee na watoto Dr. Mpoki Mwasumbi akizindua nyumba ya wauguzi katika Zahanati ya Mungere Wilayani Monduli.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa  Dr. Ellen Senkoro pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega wakishuhudia uzinduzi wa Nyumba za wauguzi wa Zahanati ya Mungere katika Wilaya ya Monduli.
Mtendaji Kuu wa Taasisi ya Mkapa Dr. Ellen Senkoro akimkabidhi cheti cha ukamilifu wa ujenzi wa Nyumba 20 za wauguzi zilizopo Mkoani Arusha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dr. Mpoki Mwasumbi.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dr. Mpoki Mwasumbi akimkabidhi cheti cha ukamilifu wa ujenzi wa nyumba 20 za wauguzi Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,nyumba hizo zimajengwa na taasisi ya Mkapa kwaniaba ya Wizara.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega akimkabidhi rasmi Mkurugenzi wa Wilaya ya Monduli Oye Nguyaine nyumba 20 za wauguzi kwa mkoa wa Arusha.

Nyumba hizo 10 zimejengwa katika Wilaya na Monduli na 10 nyingine katika Wilaya ya Ngorongoro ambapo kila moja imegharimu milioni 53.

Ujenzi huo umekamilika chini ya usimamizi wa taasisi ya Mkapa na wakandarasi waliofanya kazi ya ujenzi huo ni kampuni zilizopo Mkoani Arusha.

Mbali na ujenzi wa nyumba hizo 20 kwa mkoa wa Arusha, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ameiomba taasisi ya Mkapa kuongeza nyumba nyingine 20 kwa Wilaya nyingine za Mkoa wa Arusha ikiwemo Wilaya ya Longido.

Taasisi ya Mkapa ilianza mradi wa ujenzi wa nyumba za wauguzi mnao mwaka 2013 na unatarajia kujenga nyumba 480 kwa nchi nzima ikiwa ni ushirikiano wake na serikali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni