BOSI WA KUNDI LA MAFIA LA ITALIA BERNARDO PROVENZANO AFARIKI DUNIA GEREZANI

Bosi wa kundi la mafia la Italia Bernardo Provenzano amefariki dunia akiwa hospitali ya gereza akiwa na umri wa miaka 83.

Provenzano, maarufu kama "The Tractor" kutokana na ukatili wake, alikamatwa na kufungwa mwaka 2006, baada ya kuwapiga chenga polisi kwa miaka 43.

Provenzano alitwaa madaraka ya kuliongoza kundi la Mafia la Sicilian mwaka 1993, baada ya kukamatwa kwa aliyekuwa bosi wao Salvatore "Toto" Riina.

Provenzano alikuwa anatumikia kifungo cha maisha kutokana na kufanya mauaji kadhaa, wakiwemo majaji waandamizi wa kesi za Mamafia Giovanni Falcone na Paolo Borsellino.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni