Wabunge
wa chama cha Conservative wamesimama wima wote bungeni ikiwa ni
heshima kwa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron baada ya kumaliza
kipindi chake cha mwisho cha maswali na majibu kabla ya kuachia
madaraka.
Waziri
Mkuu Cameron, baadaye leo ataenda kwenye makazi ya malkia huko
Buckingham Palace, kuwasilisha rasmi barua yake ya kujiuzulu wadhifa
wake kwa Malkia Elizaberth wa pili.
Akitetea
mafanikio yake akiwa madarakani Cameron amesema kilikuwa ni kipindi
mambo yenyekuvutia wakati wote wa miaka sita iliyopita akishikilia
wadhifa huo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani Theresa May, anajianda kuchukua madaraka kutoka kwa
Cameron baadaye baada ya kukutana na Malkia.
Wabunge wa Conservative wakiwa wamesimama juu na kupiga makofi wakimuaga Waziri Mkuu David Cameron
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni