Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati akikagua ujenzi wa
kiwanda cha vigae cha Goodwill Ceramic kwenye kijiji cha Mkiu wilayani
Mkuranga Julai 13, 2016,Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi
Evarest Ndikilo na kulia ni Balozi wa China nchini, Dkt Lu Youqing.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa
Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing (wapili kulia) kwa ajili ya
madawati wakati alipokagua ujenzi wa kiwanda cha vigage cha Goodwill
Ceramic kinachojengwa katika kijiji cha Mkiu wilayani Mkuranga Julai 13,
2016. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage,
Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandishi Evarest
Ndikilo na kulia ni Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega.
Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa akipongezana na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega
baada ya kupokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa Balozi wa China
Nchini, Dkt. Lu Younqing kwa ajili ya madawati baada ya kukagua ujenzi
wa kiwanda cha vigae cha Goodwill Ceramic kilichopo katika kijiji cha
Mkiu wilayani Mkuranga Julai 13, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumzana Balozi wa China Nchini , Dkt. Lu
Youqing (wapili kulia) , Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage
(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo (kushoto)
baada kukagua ujenzi wa kiwanda cha vigae cha Goodwill na kuzungumza na
wananchi kwenye kijiji cha Mkiu wilayani Mkuranga Julai 13, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa
Lindi, Ali Mtopa baada kuwa kuwasili mjini Lindi Julai 13, 2016 kwa
ziara ya kikazi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mama Salima Kikwete, mke wa Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne baada ya kuwasili mjini Lindi kwa ziara ya
kikazi Julai 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni