Viongozi
wakuu na waandaaji wa mashindani ya mbio za Magari wakiwa katika
mkutano huo wa waandishi wa habari leo Juni 30 Jijini Dar es Salaam
katika hotel ya Southern Sun.
Kamishna
Msaidizi wa jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda
Fortunatus Musilimu akizungumza katika mkutano huo ambapo alimwakilisha
Kamanda Mpinga. Jeshi hilo limebainisha kuwa watazingatia sheria za
usalama barabarani
Meneja
Masoko na mauzo wa kampuni ya Radio Wave Communications, Bi. Suraiya
Ismail ambao pia ni wadhamini wa mashindano hayo ya magari akizungumza
katika tukio hilo. Kushoto ni Meneja mauzo wa Mkoa wa kampuni ya Utrack
Africa Ltd, Bi.Mary Cassian
Meneja Masoko na mauzo wa kampuni ya Radio Wave Communications, Bi. Suraiya Ismail akizungumza katika tukio hilo.
Waandaaji
Wakuu wa shindano hilo kampuni ya Oryx Energies, Mkurugenzi Mkazi
Tanzania, Bwana Nick McAleer akizungumza katika tukio hilo. (Picha zote
na Andrew Chale, Modewjiblog).
Mashindano ya magari yanayojulikana kwa jina la Oryx Ernegies Rally of Tanzania 2016 yanatarajiwa kufanyika Julai 8 mpaka 10 mwaka huu huko Bagamoyo Mkoani Pwani huku jumla ya magari 25 yatashindana.
Wakitambulisha rasmi tukio hilo kwa vyombo vya Habari, Waandaaji Wakuu wa shindano hilo kampuni ya Oryx Energies kupitia kwa Mkurugenzi Mkazi Tanzania, Bwana Nick McAleer amebainisha kuwa kampuni yao yao hiyo imejiandaa vyema kupitia mashindano hayo na yatakuwa ni ya aina yake siku hiyo hivyo wananchi waendelee kutumia bidhaa za Oryx ikiwemo mafuta, virainishi vya magari, gesi na bidhaa zingine kutoka kampuni hiyo ambayo vinapatikana hapa Tanzania.
“Mashindano ya Oryx Energies Rally of Tanzania 2016 ni miongoni mwa michezo bora na mizuri yenye kuvutia. Hivyo jamii itapata nafasi ya kushuhudia michuano hii mwishoni mwa wiki kuanzia Julai 8 hadi 10 mwaka huu katika viunga vya Bagamoyo” alieleza Mkurugenzi Mkazi huyo, Bwana Nick McAleer.
Kwa upande wake Bi. Surayia kutoka kampuni ya U track and Radio Wave ambao wanahusika na masuala ya vifaa vya mawasiliano na ulinzi katika magari ambao pia ni miongoni mwa wadhamini kwenye mashindano hayo wamesema kuwa vifaa bora na vya kisasa vitatumika wakati wa mashindano hayo ikiwemo kubaini gari lililopotea njia ama kuharibika na kutoa msaada wa haraka katika mashindano hayo.
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania, Bwana Mohamed Kiganja akizungumza kwa upande wa Serikali amesema kuwa, ametaka kuona vyama vya michezo vinasonga mbele na kuacha kufanya kazi kwa mazoea licha ya kukabiliwa na changamoto za uendeshaji.
Kiganja amebainisha kuwa, chama cha mbio za magari kimekuwa kikijitahidi kufanya shughuli zake mbalimbali hivyo kuwa na maendeleo tofauti na vyama vingine ambavyo vilitakiwa kuiga mfano huo.
“Tuache mazoea hizi sasa ni zama za Hapa Kazi tu. Vyama vya michezo vijikite kufanya shughuli za kijamii ili zionekane kwani ndio majukumu yao na sio kusubiria mashindano tu, Sasa kama hakuna mashindano nini kitafuata?, si ndio mwanzo wa kuanza kugombana maana vyama hivi vikipataa pesa tu ugomvi unaingia” alibainisha Kiganja.
Kiganja pia alipongeza mashindano hayo ya Mgari na kubainisha kuwa, mchezo huo wa Magari ni miongoni mwa michezo bora kabisa hapa nchini hvyo inatakiwa kuungwa mkono na pande zote kama michezo mingine huku akiwataka waandaaji wake kuhakikisha wanaipeleka mbio hizo za magari katika mikoa mingine ya Tanzania ikiwemo Mwanza ambapo wageni mbalimbali wanaweza kushiriki hasa kutoka nchi za jirani.
Kwa upande wake, Rais wa chama cha Magari Tanzania (AAT), Bwana Nizar Jivani amesema kuwa, mashaindano hayo yamezingatia viwango vyote ambapo jumla ya magari 25 yatashiriki ambapo kati ya magari hayo, Magari 4 yatatoka Uganda, 2- Zambia, Kenya (1), Falme za Kiarabu (1). Na kwa magari ya kutoka Tanzannia ni 17.
Magari hayo 17 ya Tanzania ambapo Dar es Salaam magari 10, Arusha (3), Moshi (3), na Tanga (1). Aidha, magari hayo yanatarajiwa kushindana katika umbali wa kilometa 246 kwa siku ya kwanza.
Uzinduzi huo unatarajiwa kuzinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye katika hoteli ya Southern Sun Dar es Salaam, siku hiyo ya Julai 8.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni