Micah Johnson, mtuhumiwa anayedaiwa
kuwauwa maafisa polisi watano kwa risasi katika maandamano huko
Dallas nchini Marekani inasaidikiwa alitenda tukio hilo akiwa peke
yake.
Akiongelea tukio hilo lililotokea
wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya Wamarekani weusi, Meya Mike
Rawlings amesema wanaamini kwa sasa mji wa Dallas upo salama.
Vifaa vya kutengenezea bomu, bunduki
aina ya rifle na jarida la kombati vilikutwa nyumbani kwa Johnson
ambaye aliwahi kulitumikia jeshi la Marekani nchini Afghanistan.
Johnson ambaye aliuwawa kwa bomu la
roboti, kabla ya hapo aliwaambia polisi amechoshwa na mauaji ya watu
weusi yanayofanywa na polisi, hivyo analipa kisasi kwa kuwauwa polisi
weupe.
Polisi wakitoka na vitu kwenye nyumba ya Micah Johnson
Aina ya bunduki aliyotumia Micah Johnson kuwadungua kwa risasi polisi
Micah Johnson kulia akiwa na kaka yake Tevin na mdogo wao wa kike Nicole
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni