Mkuu
wa wilaya ya Moshi Kipi Warioba akiongozana na kundi la wapanda mlima
Kilimanjaro kutoka kampuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining (GGM)
waliopanda kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia taasisi mbalimbali
zinazo shughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi.
Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM) ,Simon Shayo akizungumza
wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya kundi la wapanda mlima wakiwemo
wafanyakazi wa mgodi huo waliopanda kwa leongo la kuchangisha fedha za
kusaidia taasisi mbalimbali zinazo shughulika na mapambano dhidi ya
Ukimwi.
Kiongozi
wa kundi la wafanyakazi wa kampuuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining
,Kelvin Yasiwa akizungumza kwa niaba ya wenzake mara baada ya kuwasili
wakitokea katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Balozi
wa Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Msanii Mrisho Mpoto
akizungumza mara baada ya kurejea salama kutoka katika kilele cha Mlima
Kilimanjaro.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba akikabidhi cheti kwa mtoto
Lucy Mashauri(15)baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima
Kilimanjaro.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba akikabidhi cheti kwa mtoto
Jacob Musa (16) baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima
Kilimanjaro.
Balozi
wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Msanii Mrisho Mpoto
akifurahia baada ya kukabidhiwa cheti kwa kufanikiwa kufika katika moja
ya vilele vya Mlima Kilimanjaro,kilele cha Stela .
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba
akikabidhi vyeti kwa washiriki wengine wa changamoto hiyo ya kupanda
Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia taasisi
mbalimbali zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya Ukimwi.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba
aliyekua mgeni rasmi katika hafla hiyo Kipi Warioba akizungumza mara
baada ya kuwapokea wapandaji wa Mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya
Mgodi ya Geita Gold Mining.
Washiriki
wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengoo la kuchangisha
fedha kwa ajili ya kusaidia taasisi mablimbali zinazojishughulisha na
mapambano dhidi ya Ukimwi wakifungua "champagne" kuonesha furaha mara
baada ya kurejea salama kutoka katika kilele cha Mlima Kilimannjaro.
Washiriki
wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha
fedha kwa ajili ya kusaidia taasisi mbalimbali zinazojihusisha na
mapambano dhidi ya Ukimwi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
wa hafla ya mapokezi yao,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni