ICELAND YAPOKELEWA KISHUJAA BAADA YA KUTOLEWA HATUA YA ROBO FAINALI

Wachezaji wa timu ya soka ya Iceland wamepokelewa kishujaa baada ya kurejea kutoka katika michuano ya Euro 2016, huku maelfu ya mashabiki wao wakiwa mitaani ya mji Reykjavik
kuwashuhudia.

Timu hiyo ilienda Ufaransa ikiwa ni moja ya taifa dogo kabisa kuwahi kushiriki michuano ya Euro, likiwa na wananchi wapatao 332,529.

Hata hivyo Iceland haikujali ugeni wala udogo katika michuano hiyo kwani ilifanya vyema hadi kutinga robo fainali ambapo ilitolewa na Ufaransa kwa magoli 5-2.
         Wachezaji wa Iceland wakiwa juu ya basi lao wakishangiliwa na mashabiki wao 
Wachezaji wa Iceland wakiwapungia mikono mashabiki wao kuwashukuru kwa mapokezi makubwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni