Mtoto
wa kiume aliyewezeshwa na rais Uhuru Kenyatta kusafiri India kwa
matibabu ya kupandikizwa figo amekwama nchini humo baada ya familia
yake kushindwa kupata shilingi milioni 2.8 za Kenya ili kulipia bila
ya hospitali.
Hospitali
ya Artemis iliyopo Haryana inashikilia hati za kusafiria za mama na
mtoto huyo Brian Karuga na Bi. Ruth Njeri, pamoja na nyaraka nyingine
mbalimbali za kusafiria tangu Juni 20, mwaka huu.
Bi.
Njeri amesema walilazimishwa kukabidhi nyaraka hizo kutokana na
kutokuwa na kiasi chote cha shilingi milioni 6 za Kenya zilizokuwa
zinahitajika na hospitali hiyo ya India kwa ajili ya gharama za
matibabu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni