Nyota
wa Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) wameomba kumalizika kwa matukio ya
mauaji ya kutumia bunduki pamoja na mauaji yanayofanywa na polisi
yenye mrego wa kibaguzi kwa weusi nchini humo.
Wito
huo umetolewa na nyota wa kikapu LeBron James, Carmelo Anthony, Chris
Paul na Dwyane Wade katika hutuba yao wakati wa hafla ya utoaji Tuzo
kwa Wanamichezo Bora wa mwaka (ESPY) Jijini Los Angels.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti kufuatia matukio ya hivi karibuni ya kuuwawa na
polisi Wamarekani weusi wawili, nyota hao wa kikapu wamesema
imetosha sasa na ni wakati wa kukomesha mauaji ya aina hiyo.
LeBron James akiongea kwa hisia kali katika hafla hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni