KOCHA CLAUDIO RANIERI AMTAKA N'GOLO KANTE KUFANYA MAAMUZI HARAKA

Kocha Claudio Ranieri amemtaka mchezaji N'Golo Kante afanye maamuzi ya haraka juu ya mstakabali wake ili kuiwezesha Leicester kujipanga vyema iwapo mchezaji huyo raia wa Ufaransa ataamua kuhama.

Timu ya Chelsea inajiamini kunasa saini ya kiungo huyo mkabaji kwa uhamisho wa kitita cha paundi milioni 30, lakini Leicester nao wameshampatia ofa ya mkataba mpya mchezaji huyo na kusisitiza kuwa hakuna makubaliano yaliyofikiwa.

Sasa kocha Ranieri anataka kila kitu kiwe wazi wakati Leicester ikianza mchezo wake wa kirafiki wa kujiandaa na Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Oxford siku ya jumanne wakati akianza kukinoa kikosi hicho kutetea taji la Ligi Kuu ya Uingereza.
Kiungo Mkakamavu N'Golo Kante anawakati mgumu kuamua kati ya kubaki Leicester ama kuhamia Chelsea

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni