Mdunguaji amewapiga risasi na
kuwauwa polisi wanne na kujeruhi wengine saba huko Dallas, Marekani
katika maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi yanayofanywa na
polisi.
Milio ya risasi ilisikika wakati
waandamanaji walipokuwa wakiandamana katika mji huo. Mtu mmoja
anashikiliwa na polisi na mwingine mmoja aliyeonekana na bunduki
amejisalimisha.
Polisi wakiwa kazini wakimsaka mdunguaji
Hali ilikuwa inatisha kiasi ya watu kujificha kwenye magari wakati polisi wakihaha kumsaka mdunguaji
Huyu aliamua kundamana na bunduki yake, na sasa amejisalimisha polisi kwa mahojiano zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni