Waziri
wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na viongozi wa
Kampuni ya Uchimbaji Madini ya mkoani Geita (GGM) pamoja na Viongozi wa
Serikali wa mkoa huo, kuhusiana na masuala mbalimbali ya utatuaji wa
migogoro iliyopo kati ya GGM na wananchi wanaoishi jirani na mgodi huo.
Waziri Mwakyembe aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, katika ziara hiyo. Picha zote na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza
jambo katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu
Ezekiel Kyunga (katikati), na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison
Mwakyembe (wa tatu kushoto) mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili
ya ziara ya kikazi zilizofanywa na viongozi hao wa Wizara. Wapili
kushoto ni Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga. Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Geita (GGM), Terry MulPeter
akizungumza katika kikao kati ya uongozi wa kampuni yake na viongozi wa
serikali uliokuwa unaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison
Mwakyembe na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (hawapo pichani). Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza
jambo katika kikao cha viongozi wa serikali pamoja na viongozi wa
Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Geita (GGM) cha kujadiliana masuala
mbalimbali ya utatuzi wa migogoro kati ya kampuni hiyo na wananchi
wanaoishi jirani na kampuni hiyo. Kikao hicho ambacho kiliongozwa na
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (wanne kulia) ambacho
kilifanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. Watatu kulia ni Mkuu
wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga. Wa pili kulia ni
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia), Mkuu wa
Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kushoto kwa Dk
Mwakyembe), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (katikati ya Dk Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa) pamoja na viongozi
wengine wakitoka kulikagua Bweni la Mahabusu la Gereza Chato
linalojengwa mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza
jambo ndani ya Bweni la Mahabusu la Gereza Chato linalojengwa mkoani
Geita. Wapili kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe
ambaye alikuwa kiongozi wa msafara huo. Kushoto ni Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu, Edward Kaluvya. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi
wa Mashtaka, Biswalo Mganga (aliyevaa kaunda suti) akichomolewa ndani
ya gari lake lililopinduka katika Kijiji cha Bwanga wilayani Chato, Mkoa
wa Geita, wakati dereva wa gari hilo alipokuwa anamkwepa mwanafunzi
aliyekatisha ghafla barabarani wakati wa msafara wa ziara ya kikazi wa
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (kulia aliyevaa kofia)
na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(hayupo pichani). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari mjini Chato, mkoani Geita mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yao na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto). Katika ziara yao licha ya kufanya majukumu mengi ila walifanikiwa kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini mkoani Geita (GGM) na pia walilikagua Gereza Chato linalojengwa mkoani humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni