WATU WENYE SILAHA WAVAMIA KITUO CHA POLISI KENYA NA KUUWA POLISI

                                   Mkuu wa Kituo cha polisi Kapenguria (OCS) Vitalis Ochido

Maafisa polisi watano wanahofiwa kufa nchini Kenya baada ya watu wenye silaha kushambulia kituo cha polisi huko Kapenguria, magharibi mwa Pokoti, leo alfajiri.

Watu hao wenye silaha walivamia kituo hicho ili kuwakomboa wenzao waliokamatwa eneo la Nakujit kwa tuhuma za kuwa ni magaidi.

Taarifa zaidi zinasema mkuu wa kituo hicho cha polisi (OCS) Vitalis Ochido inasemekana kuwa amejeruhiwa katika shambulizi hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni