Dk. Kigwangalla amebainisha hayo katika ziara yake ya kushukuru wananchi wa Jimbo hilo la Nzega Vijijini kwa kumuwezesha kumchagua kurudi Bungeni kwa kura nyingi na pia kumpigia Rais Magufuli kwa kula za kutosha kuingia madarakani
“Ndugu zangu wananchi wa Kata ya Milambo Itobo na wale wa Kata ya Magengati …Leo narejea hapa kuwashukuru kwa kunichagua kwenu. Nashukuru sana kwani kula zenu zimeweza kuniwezesha mimi kwa mara nyingine tena kurejea Bungeni na kuweza kuwawakilisha nyie katika vikao vya maamuzi hasa vile vya kimaendeleo. Na kutokana na uchapaji wangu wa kazi hata Rais ameniona mimi ni jemba na amenipatia moja ya nafasi za Uwaziri.
ameniteua kwenye Baraza lake la Mawaziri. Napenda kuwapongeza sana na pia naomba niwafikishie salama za Rais kwa kuweza kumpatia kura nyingi sana za NDIO…” Alieleza Dk. Kigwangalla katika mkutano huo wa wazi ambao watu mbalimbali walipata wasaha wa kushuhudia mkutano huo wa kutoa shukrani ambapo pia alitoa misaada mbalimbali ambayo aliahidi yeye mwenyewe kwa moyo wake hasa kwa vijana.
Aidha, Dk. Kigwangalla aliwaomba wananchi wa Vijiji vya Kaloleni kuwa na subira kwani atahakikisha Umeme wa gridi ya Taifa inapita katika vijiji hivyo na kupata umeme wa uhakika ambapo kwa sasa tayari ameliombea hilo na litatekelezwa muda wowote kuanzia sasa.
Mbali na hilo pia aliwataka wananchi wa Jimbo hilo la Nzega Vijijini kuwa na subra kwa kipindi hiki kwani barabara inayoanzia kwenye barabara kuu ya lami ya Tabora kuingia Inagana mpaka Milambo Itobo ambayo hipo chini ya Tanroad, inatarajiwa kukarabatiwa na itakuwa msaada kwa wakazi wa maeneo hayo ambao wengi wao wanajishughulisha na shughuli za Kilimo ikiwemo ulimaji wa vitunguu kwa wingi, Tumbaku, Pamba na Mpunga.
Mbali na kutoa ahadi hizo kwa wananchi hao, Pia Dk. Kigwangalla aliahidi kutoa shilingi Laki tatu kwa vijiji vya Kaloleni, Usagali na Inagana kwa ajili ya kuchangia maswali ya dini
Dk. Kigwangalla pia mbali na kutoa shukrani kwa wapiga kula wake hao, pia alipata wasaha wa kusikiliza kero za wananchi huku akipokea kero zao hizo ambapo ameeleza kuwa atazifanyia kazi
Wananchi waliuliza maswali mbalimbali ikiwemo kupata matibabu licha ya kujiunga na mfumo, barabara mbovu, Umeme. Na Andrew Chale, Nzega
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni