MICHELLE OBAMA AMPONDA DONALD TRUMP, NA KUMUUNGA MKONO BI. CLINTON

Michelle Obama mke wa rais wa Marekani amemponda mgombea urais wa Republican Donald Trump, na kumuunga mkono Hillary Clinton katika mkutano wa Taifa wa Chama cha Democratic huko Philadelphia.

Huku akishangiliwa na kupigiwa makofi na wajumbe wa mkutano huo Michelle Obama amesema lugha za chuki zinazotolewa na watu mashuhuri kwenye TV, haziwasilishi moyo wa uzalendo wa taifa hilo.

Kama hiyo haitoshi Michelle amewataka wafuasi wa chama cha Democratic kutojishusha sawa na wapinzani wao, kwani kauli mbiu ya chama hicho ni “Wao wakijishusha, sisi tunakwenda juu”.
Awali aliyekuwa mshindani mkuu wa Bi. Clinton, Seneta Bernie Sanders amewasihi wafuasi wa chama cha Democrat, kumuunga mkono Bi. Hilary Clinton.
Wanachama wa Democrat wakimshangilia Michelle Obama wakati akitoa hotuba yake
Michelle Obama akionyesha ishara ya vidole gumba baada ya kumalizi kutoa hotuba yake

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni