SHULE ya
Sekondari Kisimiri iliyoshika nafasi ya kwanza Kitaifa kwa matokeo ya kidato cha sita iliyopo
wilayani Arumeru ,Mkoani Arusha inahitaji shilingi milioni 900, kwa ajili ya ujenzi wa
uzio na mabweni ili kuwanusuru wanafunzi wanao ishi shuleni hapo wasiliwe na
wanyama wakali wanao randa randa nyakati za usiku .
Hayo yalibainishwa
mwishoni mwa wiki na mkuu wa shule hiyo mwl,Emmanuel Kisongo alipo tembelewa na
,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru , Japhet Kazeri kwa lengo la kumpongeza na
kumkabidhi cheti maalumu baada ya kuitoa kimaso maso Halmashauri yake.
Kisongo
alisema kuwa shule hiyo pamoja na kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani, haijawai
kupewa msaada wowote na serikali ila jitihada za waalimu zimesaidia kuifikisha
shule hiyo ilipo na kufanya vizuri kwa miaka 8 na kwa mwaka huu imevunja rekodi kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa
“Ni vizuri
serikali ikaangalia uwezekano wa kutusaidia hili kuondoa changamoto zinazo
tukabili tunahitaji kiasi cha shilingi milioni 900, kujenga uzio kujenga
mabweni na kukarabati miundo mbinu yetu ‘’Alisema Kisongo.
Katika hatua
nyingine Kisongo alisema kuwa tangu shule hiyo ishike namba moja Kitaifa
amekuwa akikabiliwa na changamoto nyingi kwa wazazi kuomba nafasi kuhamishia
watoto wao katika shule hiyo , pia alidai baadhi ya wamiliki wa shule binafsi
wamekuwa wakimpigia simu kumrubuni ahamie kwenye shule zao.
Aidha Kisongo
alimshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kufika katika
shule hiyo kumpongeza na kujionea
changamoto zilizopo na kueleza siri ya mafanikio ya shule hiyo pamoja na walimu
kujituma pamoja na usimamizi wake na kufuatilia mienendo za walimu juu ya
ufundishaji madarasani .
Kwa
upande
wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Japhet Kazeri, pamoja na
kuipongeza
shule hiyo kwa kuitoa kimaso maso halmashauri hiyo alikabidhi cheti
maalum kwa mkuu wa shule hiyo na kuahidi kutatua changamoto ya bara
bara yenye urefu wa kilometa 7 inayo elekea shuleni
hapo kwa kutengeneza katika kiwango cha changarawe .
Hata hivyo
alisema ni jukumu la serikali kutunza mazingira na miundo mbinu za shule zinazo
fanya vizuri hasa katika matokeo ya mitihani.
Kwa upande
wake Afisa elimu wa shule za sekondari wa halmashauri hiyo mwl. Damari Mchome alisema
tangu shule hiyo kuibuka kinara wa ufaulu kitaifa ofisi yake imepokea maombi ya
barua zaidi ya 700 kwa wazazi kuomba watoto wao kuhamia katika shule hiyo.
Mchome
alisema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 1117 na walimu 68 kwa sasa haina nafasi
ya kuchukua wanafunzi wapya huku akiwataka wazazi wawe na subira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni