Makamu
wa Rais wa Huduma wa Shirika la Ndege la Etihad, Sajida Ismail, Makamu
wa Rais wa Uhusiano wa shirika hilo, Calum Laming akipokea tuzo za
Skytrax World Airline ya World Best First Class Airline, World’s Best
First Class Onboard Catering na World’s Best First Class Airline Seat
Shirika
la ndege la Etihad limetunukiwa tuzo tatu za ubora wa juu kwenye
madaraja pia tuzo ya ubora kwenye huduma za vyakula pia tuzo ya ubora
kwenye malazi kutoka Skytrax Worldairline Awards, zilizotangazwa NCHINI
uingereza.
Tuzo
hizo za World Airline ni za kimataifa na huhusisha mashirika ya ndege
yanayofanya vizuri katika sekta ya usafiri wa anga. Mshindi huchaguliwa
kwa kura kutokana na mchakato ambao huchukua miezi 10 kukamilika kwake
huku ikujumuisha wasafiri takribani milioni 18 kutoka katika nchi zaidi
ya 100 ulimwenguni.
Makamu
wa Rais wa Shirika la Etihad kwenye masuala ya wageni alisema,“ Mwaka
2014 tuliingia kwenye ushindani kwa kutambulisha ndege yetu ya abiria
Airbus A380 na Boing 787 Dreamliner. Jambo hili limeonyesha dhamira yetu
ya kuwa wa kwanza katika kutoa huduma ya kisasa na uvumbuzi.”
“Ninafarijika
na jambo hili ikiwa ni matokeao ya uwekezaji wa huduma bora kwa wateja
wetu ulimwenguni, kwa mara nyingine tena tumetunukiwa tuzo hizo za kuwa
wa kwanza kwa ubora katika huduma za kuwa na madaraja yenye hadhi. Tuzo
hii itakuwa chachu katika kuongeza nguvu kwenye kuwekeza zaidi kwenye
bidhaa zetu na huduma za usafiri.”
Katika
miaka ya hivi karibuni, shirika laetu limepata tuzo ya kuwa wa kwanza
kwenye huduma zetu. Hii ni mara ya pili kwa kupata tuzo na kipekee
kupata tuzo tatu kwa pamoja ikiwa ni shirika pekee kunyakua tuzo hizo.
Mwnyekiti
wa Skytrax, Edward Plaisted alisema “Shirika la Ndege la Etihad
limekuwa likiimarika na kuwa bora zaidi katika usafiri wa anga kwa
kuendana na mabadiliko ya teknolojia ya kisasa katika utoaji wa huduma
zake na ukarimu. Kwa mara nyingine tena shirika hili limenyakua tuzo
tatu muhimu kwa kupigiwa kura na amamilioni ya wasafiri ulimwenguni
kote, ambapo ni dhahili ilistahili kuwa mshindi kutokana na kutoa huduma
za kiwango cha juu.”
Kuwapo
kwa huduma nzuri za maradhi kwa wasafiri, vyumba nanae vya kulala vya
hadhi ya juu, eneo zuri na la kipekee kwa abria kupumzika likiwa na
ukubwa wa kutosha ni mambo yaliyopelekea kupata tuzo ya ubora.
Kuwapo
kwa ndege ya 787 ambayo ina ambayo imesheheni vitu mbalimbali ndani
yake ikiwamo vyumba vyenye vitanda, runinga kubwa ya kisasa, eneo la
kulia chakula na madhari ya kuvutia ni miongoni mwa mambo yaliyoipa tuzo
ya kuwa wa kwanza kwenye ubora wa hali ya juu.
Shirika
la Ndege la Etihad kwa kutumia ndege zake za Boeing 777 ana Airbus
A330/A340 itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja zikiwa na viti vyenye
mwonekano na mazingira mzuri kwa mtumiaji.
Ndege
za shirika la Etihad zimekuwa zikitoa huduma bora zaidi za hoteli ndani
ya ndege zake ili kukidhi mahitaji ya wateja wake. Katika hoteli zake
ndani ya ndege kuna huduma ya vyakula vya aina mbalimbali ambavyo
vinaandaliwa na watu wenye uzoefu. Na huduma ya chakula inatolewa kwa
madaraja yote kwenye ndege za Etihad. Pia wateja wana fursa ya
kujadiliana na watoa huduma kwenye ndege kulingana na mahitaji yao ya
chakula.
Wageni wanaweza kuchagua chakula wanachokipenda kwenye menu zinazopatikana kwenye hoteli za kwenye ndege.
Aidha
katika Uwanja wa Kimataifa wa Abu Dhabi kumefunguliwa mgahawa ambao
utahudumia wateja wa Etihad ukiwa na vitu mbalimbali muhimu ambavyo
vitakidhi mahitaji ya mteja ikiwa na lengo kila mteja apate huduma bora
inayomfaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni