Mkuu Mpya wa Wilaya ya Kahama Aanza Kazi Kwa Mkwara Mzito..Wakuu wa Idara Waishia Mlangoni

MKUU mpya wa Wilaya ya Kahama,Fadhili Nkulu,ameanza kazi ya wadhifa
wake alioteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kufanya kazi wilayani
Kahama,mkoani Shinyanga kwa kuwapiga mkwara wakuu wa Idara katika
halmashauri zote tatu kwa kuwazuia kuingia kwenye kikao chake wale
ambao walichelewa kufika katika muda uliokuwa umepangwa.

Juzi Nkulu aliwaita ofisini kwake wakuu wa Idara wote katika halmashauri
zote tatu za Mji ,Ushetu na Msalala kwa lengo la kujitambulisha na
kufahamiana na walikubaliana kikao hicho kingefanyika saa mbili asubuhi
ofisini kwake,lakini kulingana na mazoea yaliyojengeka kwa baadhi ya
watumishi baadhi yao walifika zaidi ya saa mbili .

Kufuatia hali hiyo Nkulu aliwazuia kuingia kwenye kikao hicho wale waliofika
zaidi ya saa mbili na kuwataka wakae nje ya ofisi yake,kwa kuwa
makubaliano ya mwaliko huo hayakuwa kufika zaidi ya saa mbili ingawa
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Anderson Msumba alinusulika kwenye
mkasi huo,baada ya kufika sekunde chache kabla wakati muafaka wa kikao kuanza.

“wewe umefika imezidi sekunde moja baada ya saa mbili wewe ingia
wengine watakao kuja kuanzia sasa hawataingia kwenye kikao changu
watakaa nje kusubili kutokana na kutotekeleza kufuata ratiba ya vikao
“alisema Nkulu ingawa hata baada ya kumaliza kikao chake na wale
waliowahi kufika alitoka nje na kuingia kwenye gari na kuendelea na ratiba
zake zingine .

Hali ya Mkuu huyo wa Wilaya kuwazuia kuingia kwenye kikao chake wakuu
wa Idara waliochelewa kufika imepongezwa na umoja wa wazee wa Wilaya
ya Kahama,ambapo Katibu wake,Paul Ntelya,alisema kasi hiyo ni nzuri
ambayo itawafanya wafanyakazi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea .

Ntelya alimpongeza Mkuu huyo wa wilaya kwa kasi yake hiyo na kumtaka
aendelee kuwa mkali kwenye nidhamu ya watumishi wa umma ambao wengi
wao wanafika kwenye matukio ya kazi zao kwa muda wanaotaka na si kwa
wakati unaotakiwa wengine mpaka hadi ofisini wanafika wanavyotaka.

“kwa mfano sisi wazee tulikubaliana kukutana saa nane mchana siku hiyo
lakini saa saba na nusu wote tulikuwa tumeshakusanyika iweje wao wakuu
wa Idara wakubaliane kukutana saa mbili watu wafike saa tatu mkuu huyo
yuko sahihi kabisa kuwazuia kuingia watumishi hao’’alisema Ntelya.

Nkulu ameanza kazi kahama katika uteuzi mpya wa wakuu wa wilaya
uliofanywa hivi karibuni na Rais John Pombe Magufuli na kabla ya hapo
Mkuu wa Wilaya ya Kahama alikuwa Vita Kawawa aliyeteuliwa mwaka jana
wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu na alikuja kushika nafasi ya Benson
Mpesya aliyehamishiwa Wilaya ya Songea kabla ya kusitaafu nafasi hiyo
mwaka huu .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni