Na Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI,imesema kuwa kinu cha kusaga mazao cha shirika
la taifa la usagishaji,NMC ,cha Arusha hakijauzwa kama ilivyoenezwa na
kitaendelea kuwa mali ya serikali na kwamba anaendesha kinu hicho ni mpangishaji na si vingine.
Hayo yameelezwa na msajili wa Hazina, Lawrance Mafuru,
alipokuwa akikabidhi umiliki wa kinu hicho
cha kusaga nafaka cha NMC ,cha
Arusha kutoka kwa shirika hodhi la mali za serikali, CHC,kwenda kwa bodi ya
Nafaka na mazao mchanganyiko. .
Mafuru, amesema uamuzi huo wa kukabidhi umiliki wa
kinu hicho kwa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ni maelekezo ya serikali
kwa ajili ya kukiendeleza kinu hicho na vingine vilivyopo, Mwanza, Iringa na
Dodoma.
Amesema kuwa bodi hiyo ambayo ni mmiliki mpya itakuwa
na jukumu la kukiendesha kinu hicho itapitia mkataba wa upangaji na kampuni ya
uwekezaji ya Monaban Trading Company limited kwa kuwa hiyo ni sehemu ya
biashara.
Amesema kabla
ya kukikabidhi kinu hicho kwa mmiliki mpya
walijiridhishwa kwa kufanya uhakiki wa vitu vilivyopo.
.
Mafuru,amevitaja vinu vingine ambavyo
havitabinafisishwa na vitabakia kuwa ni mali ya serikali ni pamoja na shirika
la usagishaji la taifa NMC, Mwanza, NMC,Dodoma na NMC,Iringa ,ambavyo navyo
vimekabidhiwa kwa mimiliki mpya ambayo ni bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko.
Ameongeza kuwa kinu hicho cha NMC ,Arusha, kilipangishwa
mwaka 2008 kwa kampuni ya Monaban
Trading limited,kutokana na uamuzi wa serikali uliofanywa kwa wakati huo lakini
sasa mali zote za shirika la usagishaji
la taifa hazitauzwa zitabakia kuwa mali ya serikali.
Nae Kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya nafaka na mazao
mchanganyiko, John Damasi Maige, amesema
bodi hiyo itasimamia shughuli zote za kinu hicho pia watazingatia mkataba
unaomwezesha mpangaji kampuni ya Monaban
kuendesha kinu hicho.
Amesema kuwa mara baada ya kupitia mkataba na mpangaji
ambae ni kampuni ya Monaban Trading Compan Limited,kuna mambo watakubaliana kwa
masilahi ya pande zote mbili.
Maige, amesema kuwa bodi ya nafaka na mazao
mchanganyiko inaendesha maghala yaliyopo
Dodoma, na kufufua mashine za kusagisha zilizopo NHC Mwanza,ambacho kilikuwa ni
kwa ajili ya kusagisha na kusindika
mpunga, kinu cha Dodoma kilikuwa cha kusagisha na kusindika mtama .
Lengo la kuvifufua ni kuviwezesha kufanya kazi na hivyo kutoa
ajira hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa .
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya
Monabani Trading Limited, Gerad Mandala, amesema watashirikiana na mmiliki mpya
kwa kuwa kinu hicho ni mali ya serikali na kiwanda kitaendelea kama kawaida.
Akawaondoa hofu wananchi kwa kueleza kuwa kampuni ya
Monaban ni mpangaji na ina mkataba wa muda mrefu na itaendelea kuwa msagishaji wa nafaka na
mazao mengine hivyo wananchi wataendelea kupata huduma ya unga na mahitaji
mengine kama kawaida..
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni