Na Adili Mhina
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalim
amesema kuwa serikali iko mbioni kupeleka bungeni muswada wa marekebisho
ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kutotoa mwanya kwa watoto wa kike
kuolewa katika umri wa chini ya miaka 18.
Mhe.
Ummy ameyasema hayo katika sherehe za kuadhimisha siku ya idadi ya watu
duniani ambaazo huadhimishwa tarehe 11 Julai kila mwaka.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim
(Mb) akitoa hotuba yake katika sherehe za kuadhimisha siku ya idadi ya
watu zilizofanyika Julai 11 katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar
es Salaam.
Kwa
hapa nchini, sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kuhudhuriwa na
wawakilishi mbalimbali kutoka serikalini, mashirika ya umoja wa mataifa
pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.
Katika
hotuba yake kwenye sherehe hizo zilizotawaliwa na kauli mbiu ‘wezesha
msichana afikie ndoto zake’, Waziri Mwalim alisema serikali imejipanga
vizuri kuhakikisha haki za watoto wa kike zinalindwa hivyo ni lazima
kila mwanachi aelewe umuhimu wa kumlinda mtoto wa kike na kuachana na
mila potofu.
Mkurugenzi
Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akitoa neno la
shukrani kwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya idadi ya watu
duniani.
“Hata
hivyo pamoja na sheria hizi nzuri tatizo la mimba za utotoni
halitokwisha kama jamii haitabadilika kuhusu mtizamo hasi walio nao
baadhi ya watu kuhusu wasichana. Watoto wakike wanatakiwa kuwa shuleni
na kupata taarifa sahihi za msingi kuhusu afya zao na kuondoa
unyanyapaa, “ alisema Waziri Ummy.
Waziri
Ummy alieleza kuwa kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012,
Tanzania inakadiriwa kuwa na wasichana wadogo milioni 3.4 (wenye umri
kati ya miaka 13 hadi 19) sawa na asilimia 7.6 ya watanzania wote na
hivyo idadi hii haiwezi kupuuzwa katika mipango mbalimbali ya Taifa.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe. Ummy Mwalim
akipata maelezo kutoka kwa moja ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya
idadi ya watu duniani.
Waziri
Ummy pia alitoa pongezi kwa Tume ya Mipango hususani kwa Kaim katibu
Mtendaji Bibi Florence Mwanri kwa jitihada zake za kuhakikisha masuala
ya watoto yanaendelea kutambuliwa zaidi na yanafungamanishwa na
maendeleo ya uchumi wa nchi.
“Katika
kipindi cha miaka sita niliyokaa bungeni nilikuwa sijawahi kuona waziri
wa Fedha anawekea msisitizo masuala ya kukabiliana na ndoa za utotoni
na kuyafungamanisha na maendeleo ya uchumi. Naamini hizi ni jitihada
ulizofanya kuhakikisha masuala haya yanatambulika kwa upana zaidi,
hongera sana Kaim Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kwa kazi yako
nzuri”,. Alisema Waziri Ummy.
Kaim
Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri amesema kuwa
katika kutekeleza mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa sasa
(2016/17-2020/21) unaohimiza uchumi wa viwanda ni lazima kuwekeza vizuri
kwa watoto wa kike kwa kuwa ndio nguvu kazi ya kesho inayotarajiwa
kuendesha uchumi wa viwanda.
Bibi
Mwanri alisisitiza kuwa watoto wa kike wakilindwa na kupatiwa elim
bora, taifa litakuwa na faida kubwa kwani hapo baadae wataweza
kujitegemea na kuendesha maisha yao wenyewe, vile vile wataweza kusaidia
jamaa na familia zao na pia watakuwa na mchango mkubwa katika pato la
taifa.
Kwa
sasa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa
kushirikiana na Tume ya Mipango pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu
wanaandaa utaratibu wa kutoa elim nchi nzima juu ya masuala ya watoto wa
kike hususan mimba za utotoni ili kuondokana na tatizo hilo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim
(Mb) akisaini daftari la wageni katika banda la Ofisi ya Taifa ya
Takwimu wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Idadi ya Watu
Duniani ambapo , sherehe hizo zilifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam.
Waziri Ummy Mwalim akiangalia picha na maelezo mbalimbali katika banda la Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA).
Mhe.
Ummy Mwalim akisoma jarida katika moja ya mabanda ya wadau
waliohudhuria sherehe za siku ya idadi ya watu duniani katika viwanja
vya Mnazi Mmoja, jijini Dar e s Salaam.
Kaimu
Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akimwonesha jambo
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar bw. Juma Reli wakati wa
sherehe zakuadhimisha siku ya idadi ya watu duniani.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalim
(watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
waandamizi wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa pamoja
wawakilishi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wakati wa maadhimisho
ya siku ya idadi ya watu duniani.
Waziri Ummy Mwalim (wa tatu kutoka kushoto kwa waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na wanafunzi waliohudhuri maadhimisho ya siku ya idadi
ya watu duniani. Wa kwaza kutoka kusho ni Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa
ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa, wa pili (kutoka kushoto) ni Kaim Katibu
Mtendaji Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri, wa kwanza (kutoka kulia)
ni Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar bw. Juma Reli na wapili
kutoka kulia ni Mwakilishi mkazi wa UNFPA Tanzania Dkt. Natalia Kanem.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni