BABA AUWA MKE NA BINTI YAKE KWA BUNDUKI NA KISHA NAYE KUJIUWA


Baba wa watoto watatu nchini Uingereza inaaminika amemuuwa mkewe na binti yake kwa kutumia bunduki kabla na yeye kujigeuzia mtutu na kujiuwa katika mauaji yaliyotokea nje ya bwawa la kuogelea.

Baba huyo Lance Hart, 57, inaaminika alimuua mkewe Claire Hart, 50, na binti yake Charlotte Hart, 19, majira ya saa tatu asubuhi, katika eneo la maegesho ya magari ya kituo cha The Castle Leisure huko Spalding, Lincolnshire.

Watoa huduma za dharura waliitwa baada ya waogeleaji na maafisa wa kituo hicho kusikia milio ya risasi, kabla ya kubaini mwili wa mwanaume mmoja pamoja na miili ya wanawake katika eneo la maegesho.
Magari ya polisi na magari ya kutoa huduma za dharura yakiwa katika eneo la tukio la mauaji hayo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni