Na BMG
Ni
muonekano wa milima ambayo inapatikana katika Wilaya ya Rorya mkoani
Mara, Mita chache Kutoka Mto Mara ukiwa unatoka au unaelekea wilayani
Tarime, ukitokea maeneo mbalimbali katika barabara ya Musoma-Tarime.
Maajabu ya milima ambayo iko pande zote mbili za barabara si kwamba
yanatisha, la hasha. Ni maajabu ambayo ni ya kufurahisha kiukweli
hususani ukiwa safarini ambapo ukiitazama utaona namna inavyorudi nyumba
na kufanya abiria kuhisi uumbaji wa Mungu uliotukuka katika hii dunia.
Ujenzi wa barabara iliyopinda mithiri ya nyoka katikakati ya milima hii
huifanya kuwa kivutio kingine japo kwa abiria waoga wakifika katika
milima hii sara huwa inaongezeka maana si mchezo hususani likija suala
la mpando huwa ni mpando kweli, na likija suala la mtelemko huwa ni
mtelemko kweli kwani ikiwa wewe ni muoga basi huweza hata chungulia nje
japo ukweli ni kwamba ukichungulia nje utaona uzuri wa kipekee katika
milima hiyo.
Kikubwa tunaomba shughuli za kibidanamu
zisiiathiri milima hii (mfano katika picha) maana ni tegemeo kwa
wanamara na sote twajua umuhimu wa milima kama hii ambayo ina uwepo
mkubwa wa mistu ya a
sili.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni