Mchezaji tenesi namba moja kwa
wanawake Serena Williams ametishia kuwashtaki waandaaji wa michuano
ya Wimbledon baada ya manyuyu kudondoka kwenye uwanja na nyasi
kumfanya ateleze wakati wa mchezo wake dhidi ya Svetlana Kuznetsova.
Serena aliyekuwa na hasira alisikika
akisema nitawashtaki waandaaji iwapo nitaanguka na kuumia, kauli
aliyoitoa wakati wakiwa wametoshana nguvu na mpinzani wake kwa seti
ya 5-5 katika mchezo wa raundi ya nne wa michuano yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni