Mkurugenzi
Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa akizungumza katika hafl
fupi ya kukabidhi hundi ya shs. milioni 6 kwa Mfuko wa Maendeleo wa
Kondoa (KDF) jijini Dar es Salaam itakayosaidia ununuaji wa madawati
katika Wilaya za Kondoa na Chemba mkoani Dodoma. (Picha na Francis
Dande)
Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa
Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian Majengo kwa ajili ya kununulia
madawati katika Wilaya za Kondoa na Chemba. Hafla ilifanyika jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (katikati) akizungumza
katika hafla ya kukabidhi hundi ya Shs milioni 6 kwa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF).
Mkurugenzi Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (wa pili kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya Shs. Milioni 6 Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian Majengo.
Kukabidhi mfano wa hundi.
Mkurugenzi
Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (katikati),
akimkabidhi hundi ya Shs. Milioni 6 Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian
Majengo kwa ajili ya kununulia madawati katika Wilaya za Kondoa na Chemba. Hafla
ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mweka Hazina wa KDF, Abdilay
Mvula.
Mkurugenzi Uendeshaji
wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (kulia),
akimkabidhi mfano wa hundi ya Shs. Milioni 6 Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian
Majengo kwa ajili ya kununulia madawati katika Wilaya za Kondoa na Chemba. Hafla
ilifanyika jijini Dar es Salaam.
NA MWANDISHI WETU
BENKI ya Azania Ltd imetoa madawati 75 kwa Mfuko wa
Maendeleo wa Kondoa (KDF) ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kila mwezi kutoa
sehemu ya mapato kwa ajili ya kusaidia jamii.
Akizungumza katika
hafla ya utoaji wa madawati hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya Azania, Nurdin Semnangwa, alisema: “Mwaka
huu kwa kuitikia mwito wa kilio cha
madawati kwa wanafunzi wetu wa shule za msingi na sekondari, benki ya Azania
ilidhamiria kuhakikisha wanafunzi 1,200 wanapata madawati ya kukaa.”
Aidha, Semnangwa
aliongeza: “Leo tunatoa kiasi cha shilingi milioni sita kuweza kuondoa tatizo
la kukaa chini wakati wa masomo ili
yapatikane madawati 75…kwa watoto 225 wa wilaya za Kondoa na Chemba.”
Semnangwa alisisitiza
kwamba utoaji wa madawati utaendelea katika siku za usoni kwenye mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu, Songwe na Dar
es Salaam kwani walishafanya Kilimanjaro.
“Madhumuni yetu ni
kuendelea kujitolea sehemu ya faida kwa jamii ya Watanzania wakati wowote,”
alisisitiza Mnangwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa KDF, Balozi mstaafu
Cyprian Majengo alisema: “Tunaishukuru Benki ya Azania, asasi hii imekuwa
ikishughulika na wilaya zote mbili (Kondoa na Chemba) kwa kuzingatia hilo
msaada huu utapelekwa kwenye maeneo hayo.”
“Tangu kusajiliwa
kwake (2002) asasi imesaidia mambo mengi katika kuleta maendeleo ya wilaya zote
mbili…ujenzi wa madarasa kwa kutoa vifaa vya ujenzi, kutafuta bei nzuri ya zao
la mbaazi, alizeti na ufuta, kupeleka walimu wa muda kutoka vyuo vikuu wakati
wa likizo katika shule za sekondari,” alisema Majengo.
Hata hivyo alitoa
wito kwa wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kwa wingi kuitazama jamii
hususan kwa changamoto ya sasa ya ukosefu wa madawati katika shule za msingi na
sekondari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni