MLIPUKO KATIKA TRENI WAJERUHI WATU 24 JIJINI TAIPEI NCHINI TAIWAN

Mlipuko umetokea kwenye treni ya abiria nchini Taiwan katika Jiji la Taipei na kujeruhi watu 24.

Mlipuko huo umetokea jana usiku wa manane katika stesheni ya Taipei na kuwaacha baadhi ya abiria wakiwa wamejruhiwa vibaya.

Polisi pamoja na vyombo vya ndani ya nchi hiyo walikuta behewa lililolipuka na kupasuka likiwa mabaki ya mlipuko huo.
Majeruhi aliyefungwa kwenye kitanda cha gari la wagonjwa akiwahishwa kupata huduma za matibabu
                Mmoja wa majeruhi akivuta hewa kwa kutumia mashine ya dharura ya hewa 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni