JESHI LA POLISI MBEYA LAMSHIKILIA BABA MZAZI WA KIJANA EMANUEL FEDRICK ALIYEFUNGIWA NDANI MIAKA 11


 Baba Mzazi wa kijana Emanuel Fedrick (20) mwenye tatizo la akili na viungo ,aliyejitambulisha kwa majina ya Fedrick John Mkazi wa Mwambenja Iganjo Mbeya ,ambaye anadaiwa kumfungia ndani mtoto wake kwa zaidi ya miaka 11 bila kumpatia matunzo yoyotte katika kipindi chote hicho.
Kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambeenja kata ya Iganzo mwnye tatizo la akili na mwili akiwa amelala kitandani kwa zazidi ya miaka 11 sasa
kutokona na ulemavu wake wa akili na viungo huku  wazaziwake wakishindwa kumlea vyema na kumpa huduma bora kama walivyo watoto wengine.
 
Kijana EmanueL Fedrick (20) wenye tatizo la akili akiwa amepaktwa na shangazi yake Stella John mara baada kumaliza kupatiwa chakula.
 
Na EmanuelMadafa,JamiiMojablog-Mbeya
JESHI la Polisi kupitia dawati la jinsia na watoto linamshikilia Baba mzazi wa  kijana mwenye tatizo la ulemavu wa viungo na
akili ,Emanuel Fedrick iambaye alifungiwa ndani  kwa zaidi ya miaka 11 na
wazazi wake.
Kijana huyo, mwenye umri wa miaka 20, Fredrick Emmanuel  Mkazi wa
Mwambeja Kata ya Iganjo jijini hapa amekuwa akiishi ndani bila ya kutolewa nje kwa
kipindi cha miaka 11, hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa kudhohofisha mwili wa
kijana huyo kiafya.
             
Tukio la kukamatwa kwa mzazi huyo limetokea Julai 14 ,2015 majira ya asubuhi nyumbani kwakwe katika
eneo la Mwambenja Kata ya Ilemi lililopo Jijini hapa.
 Akizungumzia hilo, Mkuu wa dawati la jinsia Mkoa wa Mbeya, Afisa wa Polisi Janet Masangano, amesema
baba mzazi wa kijana huyo Emmanuel John, anashikiliwa na polisi kwa ajili ya
mahojiano kufuatia tuhuma zinazomkabili za kumficha mtoto ndani kwa zaidi ya
miaka 11 hali ambayo imetafsiliwa kuwa ni ukatili wa kijinsia kwa motto huyo.

Amesema, sheria ya mtoto ilipitishwa na serikali mwaka wa 2009, sheria hiyo huwalinda watoto dhidi ya mazingira
hatarishi na unyanyasaji na kwamba Kama kila mtu mzima akilea mtoto mmoja,
watoto (wote) wa Tanzania watakuwa katika mazingira salama.
Amefafanua kuwa , maelezo ya awali ya wazazi wa kijana huyo, yameweka bayana kwamba walezi hao
baada ya kumuhangaikia kwa muda mrefu ya bila kupata nafuu, sasa wameamua
kumtelekeza kijana huyo na  kuamua kumfungia ndani na kumuachia mungu kama
walivyoeleza.
Akizungumzia hilo, Mwenyekiti wa mtaa wa Mwambenja, Rosemary Jama, amesema taarifa za Ferdrick
kuishi ndani ya nyumba hiyo  walikuwa nazo lakini hawakuwahi kupata
taarifa za kwamba kijana huyo hatolewi nje.
Kugundulika kwa kijana huyo kunatokana na taarifa zilizotolewa na mmoja wa wanafamilia ambaye
hakupendezwa namna kijana  huyo anavyo
hudumiwa na wazazi wa mtoto huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni