MSHAMBULIAJI ATUMIA LORI KUGONGA WATU NA KUUWA WATU 80 NCHINI UFARANSA

Watu 80 wameuwawa na wengine 100 kujeruhiwa katika mji wa Nice nchini Ufaransa, baada ya mshambuliaji kutumia lori alilokuwa analiendesha kugonga kundi la watu waliokuwa wakisherehekea Sikukuu ya kitaifa ya Siku ya Bastille.

Dereva huyo aliyetumia lori kushambulia alikuja kwa mwendo kazi na kuingia eneo ufukweni la Promenade des Anglais, na kuwagonga watu wengi waliokusanyika kusherehekea sikukuu hiyo huku wakiangalia miale ya fataki.

Polisi wa Ufaransa walifanikiwa kumpiga rirasi na kumuua dereva wa lori hilo. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amethibitisha kufa watu 80, wakiwemo watoto, huku wengine 18 wakiwa mahututi.
Polisi wakiwa wamesimama huku miili ya waliopoteza maisha ikiwa imefunikwa na kuwekwa kati kati ya barabara
   Doli la kuchezea likiwa limelazwa kando ya mwili wa mtoto aliyekufa ambao umefunikwa
Watu walionusurika wakiwa hawaamini kilichotokea wakikatiza katika eneo la miili ya iliyofunikwa
Lori lililotumiwa na mshambuliaji likiwa limeharibika kwa mbele huku likiwa na matundu ya risasi zilizofyatuliwa na polisi na kumuua mtuhumiwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni