Mawakili wakiandamana kuelekea makao makuu ya jeshi la polisi na kuahirisha shughuli zao kwenye mbali mbali mahakamani leo kama walivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha |
JESHI la polisi mkoawa
Arusha limesitisha maandamano ya wanasheria wa Chama cha wanasheria nchini TLS
kanda ya Arusha, ambao walikuwa wakipinga mwenzao kukamatwa na polisi akiwa
mahakamani akijiandaa kumtetea mteja wake.
Kaimu kamanda wa jeshi la
polisi mkoa wa Arusha,Yusufu ILembo, amesema mawaklili hao kutoka chama cha
wanasheria nchini TLS,kanda ya Arusha walitaka kuandamana kutoka mahakama kuu
kanda ya Arusha kwenda kwa kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Arusha, bila
kibali hivyo maandamano hayoyalikuwa ni batili .
Amesema kuwa mnamo Julai
22 mwaka huu wakili wa kituo cha Sheria na haki za binadamu, mkoa wa
Arusha,Yusufu Shilinde Ngalula, alikamatwa wilayani Ngorongoro, alikokwenda kutetea
mteja wake, mara baadaya kufika Ngorongoro, alikamatwa na tume ya taifa ya jeshi
la polisi na vyombo vingine vya usalama.
Alisema kuwa mara
baada ya kuhojiwa mtuhumiwa alitakiwa kurudi polisi siku ya pili na siku ya
tatu aliachiwa huru bila masharti na aliporudia kusambaza ujumbe
kupitia mitandao akidai alikamatwa na jeshi la polisi kwa siku tatu mfululizo
bila dhamana.
Amesema baada ya
kusambaza ujumbe huo jeshi la polisi wilayani Ngorongoro,lilifungua shitaka
dhidi ya wakili huyo, la kutoa taarifa za uongo kwenye mitandao
Ilembo, amesema
maandamano yeyote bila kibali ni kosa la jinai na mawakilihao wamefanya
kosahilo huku wakitambua kuwa sheria hairuhusu kuafanya maandamano bila kibali
na polisi limewaonya wasirudie tena vinginvyo watashughulikiwa
kwa mjibu wa sheria .
Amesema hakuna aliyeko
juu ya sheria hivyo kila mmoja anapaswa kulinda na kuiheshimu sheria na
polisi haitasita kumchukulia mtu yeyote hatua pindi atakapovunja sheria.
Kamanda Ilembo,amesema
tume ilipo Ngorongoro kufuatilia tuhuma dhidi ya raia mmoja wa Sweeden
SuzanChristina Nordlund, ambae amekuwa akijihusisha kuchonganishajamii za
wafugaji wilayani Ngorongoro na kishakupeleka taarifa Ulaya na Amerika kuwa
Ngorongoro sio swali na yeyekujipatia mamilioni ya fedha.
Amesema Suzan,amekuwa
akijipatia fedha mara baada ya kuanzisha migogoro kati ya makampuni mawili
ya uwekezaji ya Thomsoni na OBC, ambapo huchochea migogoro kwa wananchi ili
kuwakataa na kisha kuandika taarifa mbaya ambazo zinalenga kuzuia watalii
wasitembelee hifadhi ya Ngorongoro kwa madai kuwa sio salama.
Amesema Suzan, amekuwa
akifadhili NGOS, 30 zilizopo Ngorongoro ili kiujihusisha na migogoro hiyo ambayoinaashiriauvunjifu
wa amani na kuzuia watalii wasiingie Ngorongoro.
Kamanda, Amesema kuwa
Suzan, alishafukuzwa nchini mwaka 2010 KWA p.I,baadaya kubainika kuwa
alijihusuisha na migogoro hiyo,na alijea tebna nchini mwaka 2015 ambapo
alifukuzwa tena kwa P.I.
Amesema kuwa tayari
walimu watatu wa shule za sekondari za serikali wanashikiliwa na polisi
kutokana na kujihusisha kwao na uchochezi huo kutokana na kupokea fedha
kutokakwa Suzan kwa lengo la kuzidisha migogoro katiya wananchi na wawekezaji.
Amewataja walimu hao
kuwa niClintonMshao wa shuleya sekondari Digodigo,Sapuk Maoi, wa shuleya
srokndari Loliondo, na mwalimu Samweli Nangirya, wa sekondari ya Ngorongoro.
Amesema tume hiyo
imegundua kuwa kuna waandishi wa habari wamekuwa wakilipwa mamilioni ya fedha
na mashirika yasiyoya kiserikali wilayani Ngorongoro kwa ajiliya kuandika
taarifa za kupotosha kuhusu hali halisi ya mgogoro huo.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa chama cha wanasheria TLS,kanda ya Arusha, wakili, Akida Modesti
,amekiri kufanya maandamano hayo bila kibali na hiyo inatokana na
shinikizo kutoka kwa
mawakili ambao walitaka kumuona kamanda wa polisi mkoa ili kushinikiza mwenzao
aachiliwe.Amesema mkurugenzi huyo wa kituo cha haki za binadamu ,kituo cha
Arusha Yusufu Ngalula, alikamatwa alipokuwa kwenye mahakama ya wilaya ya
Ngorongoro, akijiaandaa kumtetea mteja wake .
Amesema kitendo hicho ni
cha uzazililishaji ndio sababu kukawa na shinikizo la kuandamana ,hadi kwa
kamanda wa polisi mkoa .
Amesema malalamiko yao
mengine ni pamoja na kupungua kwa mahusiano kati ya polisi na mawakili ambayo
yamekuwa ni ya kudharirishana hasawakili anapofika kituo cha polisi
kushughulikia maswala ya mteja wake ambae amekamatwa wamekuwa wakidhariruishwa
na kutokuthaminiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni