Wenyeji Ufaransa wamesonga mbele na
kutinga fainali za Euro 2016 kwa kupata ushindi wao wa kwanza dhidi
ya Ujerumani katika michuano mikubwa ya kimataifa tangu mwaka 1958.
Mfungaji anayeongoza kufunga magoli
katika michuano hiyo Antoine Griezmann, alitoa mchango muhimu katika
ushindi huo katika kipindi cha kwanza na cha pili kwenye dimba la
Stade de France.
Griezmann alifunga goli la kwanza
kwa mkwaju wa penati katika kipindi cha kwanza, baaada ya kiungo wa
Ujerumani Bastian Schweinsteiger kushika mpira na kushuhudiwa na refa
Muitalia Nicola Rizzoli.
Griezmann tena aliwanyanyua
mashabiki wa Ufaransa vitini na kuwahakikishia ushindi baada ya
kuachia shuti la karibu, kufuatia kipa Manuel Neuer kuokoa mchomo wa
Paul Pogba na mpira kumkuta mfungaji na kufanya matokeo kuwa 2-0.
Antoine Griezmann akipiga mkwaju wa penati uliozaa goli la kwanza
Kipa Manuel Neuer akiwa kapotea maboya na kuruka upande mwingine mpira ukitinga wavuni
Antoine Griezmann akifunga goli la pili dakika 18 kabla ya mpira kuisha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni