DONALD TRUMP AIDHINISHWA RASMI KUWANIA URAIS WA MAREKANI


Donald Trump ameidhinishwa rasmi na chama cha Republican kuwa mgombea wao wa urais wa Marekani, huku waongeaji katika mkutano mkuu wa kitaifa wa chama hicho wakimshambuliwa mno Bi. Hillary Clinton wa chama Democratic.

Bilionea Trump anatarajiwa kukubali kuteuliwa huko siku ya Alhamisi baada ya wajumbe wa majimbo wa chama cha Republican kumchagua rasmi.

Hata hivyo waongeaji katika mkutano huo walijikita zaidi katika kumshambulia muwania urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic Bi. Clinton ambaye anauwezekano mkubwa kupitishwa na chama chake.
Kutoka kushoto Donald Trump Jr, Ivanka Trump, Eric Trump na Tiffany Trump, wakishangilia matokeo ya kura alizopata baba yao
Wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa Republican wakishangilia matokeo ya kura iliyomuidhinisha Donald Trump kuwa mgombea wao

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni