Na Faki Mjaka. Maelezo Zanzibar
Shirika la Afya Duniani WHO 
limeipongeza Serikali ya Mapinduzi ya ZWanzibar na watu wake kwa juhudi 
mbalimbali walizochukua katika kukabiliana na Ugonjwa wa Kipindupindu 
nchini.
Aidha Shirika hilo limetaka 
juhudi zaidi kuendelezwa licha ya kutokuwepo kwa Mgonjwa yeyote wa 
Kipindupindu katika Kambi za kulaza wagonjwa wa Ugonjwa huo nchini 
Unguja na Pemba.
Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa 
WHO nchini Dkt. Rufaro Chatora alipotembelea Kambi kuu ya matubabu ya 
Kipindupindu huko Chumbuni Zanzibar.
Amesema hatua hiyo inatokana na 
kiwango kikubwa cha utashi wa kisiasa na kiungozi kilichooneshwa na 
Serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kukabiana na Janga hilo.
Dkt. Rufaro ametaka juhudi 
ziendelee kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha jamii inaendelea 
kuzingatia kanuni za Afya hasa utumiaji wa maji yaliyochemshwa kwa 
matumizi.
Ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya
 Zanzibar kuhakikisha wanasaidia upatikanaji wa maji safi na salama 
pamoja na usimamizi wa kanuni za Afya ili kukabiliana na Kipindupindu.
Aidha Dkt. Rufaro Amemuhakikishia
 Waziri wa Afya kuwa Shirika lake litaendelea kushirikiana na Serikali 
katika kupambana na magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa yakichochewa na 
Mabadiliko ya Tabia nchi na ukuwaji wa Miji.
Kwa upande wake Waziri wa Afya 
Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amelishukuru Shirika la Afya na Wadau 
wengine kwa juhudi zao ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na 
Ugonjwa wa Kipindupindu nchini.
Amesema licha ya hali kuimarika 
lakini njia pekee ya kulimaliza tatilo la kipindupindu kwa ujumla wake 
ni kuhakikisha mazingira ya Zanzibar yanakuwa safi muda wote.
Amesema Serikali inaendelea 
kuruhusu Wafanyabiashara waliotimiza masharti ya Afya kuendeleza 
biashara zao na kwamba Wafanyabiashara wengine wanatakiwa kufuata 
utaratibu huo.
Jumla ya Watu 68 Zanzibar 
wamepoteza maisha yao kutokana na Ugonjwa wa kipindupindu na Wagonjwa 
zaidi ya 4,320 walilazwa katika kambi mbalimbali za ugonjwa huo Unguja 
na Pemba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni