Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla,akitolea ufafanuzi na kujibu
kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi wa Mkoa wa Mbeya, katika kikao
maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Mkapa, ambapo kubwa zaidi katika siku hii, Makala amesema
serikali itahakikisha inamkamata mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege
wa Songwe kutoka kampuni ya Kundan Sigh, baada ya kushindwa kulipa
mafao ya vibarua zaidi ya 50.
Na Emanuel Madafa, Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameagiza kukamatwa kwa mmiliki
wa kampuni ya Kundan Singh, ambaye alipewa tenda ya kujenga uwanja wa
ndege wa Songwe, baada ya kushindwa kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa kauli hiyo , wakati akijibu na
kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa
kipindi kirefu, hali iliyochangia wananchi kuichukia serikali kwa madai
ya kushindwa kuwatendea haki.
Awali, akitoa malalamiko hayo kwa Mkuu wa Mkoa, Joshua Mwasilonde
kwa niaba ya vibarua wenzake, amesema wamekuwa wakidai mafao yao tangu
mwaka 2012/2013 katika mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF na kwamba kila
wanapofuatilia wamekuwa wakipigwa kalenda.
Akilizungumzia hilo, Makala amesema, kwakua serikali iliingia
mkataba na kampuni hiyo na kumalizana nayo bila ya kuacha deni lolote
hivyo mkandarasi huyo anapaswa kuwalipa vibarua hao na kuutaka uongozi
wa NSSF, kuhakikisha unavishirikisha vyombo vya dola katika kumkamata
mkandarasi huyo.
Meneja NSSF Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Robert Kadege,
akilitolea ufafanuzi suala hilo, amesema suala la vibarua hao
linafanyiwa kazi na kwamba tayari mahakama imetoa hukumu na kuupa
ushindi mfuko huo.
Katibu tawala Mkoa wa Mbeya Mariam Mtunguja, akitolea ufafanuzi baadhi ya masuala ya kiutendaji katika kikao hicho.
Baadhi ya wananchi waliofika kutoa kero na malalamiko katika kikao hicho.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali katika kikao maalum
cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
Mkapa June 29 mwaka huu.
Baadhi ya wananchi wakitoa malalamiko na kero zao katika kikao
maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Mkapa June 29 -2016 ambapo MKuu wa Mkoa wa Mbeya Amos
Makalla ndiye aliyepokea kero hizo sanjali na watendaji wa serikali na
taasisi mbalimbali za serikali.
Kikao kikiendelea.(Picha E.Madafa).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni