Na Greyson Mwase
Serikali
imesema wawekezaji wazawa wana haki ya kuwekeza kwenye sekta za mafuta
na gesi ili sekta hizo ziwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa
nchi.
Hayo
yamesemwa na mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na
Madini Mhandisi Petro Marwa kwenye maonesho ya kimataifa ya sabasaba
yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhandisi
Petro alisema kumekuwepo na dhana kuwa wawekezaji kutoka nje ya nchi
wanapewa kipaumbele katika uwekezaji kwenye gesi na mafuta jambo ambalo
si sahihi.
Alisema
ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania ananufaika na uwekezaji kwenye
sekta za gesi na mafuta, Serikali imeweka sheria nzuri za kuwezesha
watanzania kuwa sehemu ya uchumi wa gesi na mafuta.
“
Kwa mfano Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 kifungu cha 218 kinaeleza
ushiriki wa serikali kupitia Kampuni ya Mafuta ya Taifa (National Oil
Company) na kifungu cha 219 na 220 kinaainisha ushiriki wa watanzania
katika utoaji wa huduma na bidhaa kwa makampuni yaliyowekeza nchini
kwenye sekta za mafuta na gesi,” alisema Mhandisi Petro.
Mhandisi
Petro aliendelea kusema kuwa serikali imeweka mikakati mbalimbali
kuhakikisha watanzania wanakuwa si watazamaji kwenye uvunaji wa
rasilimali za gesi na mafuta bali wanakuwa ni washiriki kamili na
kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Akielezea
mikakati hiyo, Mhandisi Petro alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya
Nishati na Madini ilianzisha kozi mbalimbali zinazohusu mafuta na gesi
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
na Chuo cha Madini (MRI).
Aliongeza
kuwa Wizara imekuwa ikiwezesha wanafunzi wanaofanya vizuri katika
masomo ya sayansi kupata ufadhili wa kusomea masuala ya mafuta na gesi
katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Mhandisi
Petro alitoa wito kwa watanzania wote kuchangamkia fursa zilizopo
katika sekta za mafuta na gesi ili nchi iweze kutoka kwenye kundi la
nchi masikini duniani na kuingia katika orodha ya nchi zenye kipato cha
kati ifikapo mwaka 2025 kama Dira ya Maendeleo ya Taifa inavyofafanua.
Afisa
Habari, Mhandisi Yisambi Shiwa (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa
Madini Nchini (TMAA) akielezea madini ya dhahabu yanavyochenjuliwa kwa
mteja aliyeshika sampuni ya madini hayo kwenye banda la TMAA katika
maonesho hayo.
Mtaalam
kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Phillip Mathayo (kushoto) akielezea
majukumu ya Wizara kwa mteja aliyetembelea banda hilo katika Maonesho
ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam International Trade Fair)
yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washiriki
kutoka Kampuni ya Kuendeleza Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC)
wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba
(Dar es Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja
vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa wateja (kushoto) akitoa maoni yake kwenye banda la Shirika la Madini
la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es
Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washiriki
kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakiwa katika picha ya
pamoja kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam
International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Neema
Mwambenja kutoka Taasisi ya Environmental Foundation for Tanzania
(EFFORT) ambayo ni mdau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) (katikati)
akitoa maelezo ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo kwenye banda la
REA, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam
International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Odriana Magige kutoka taasisi
hiyo.
Mhandisi
Migodi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Suleiman Khalid
(katikati) akielezea shughuli zinazofanywa na shirika hilo. Kushoto ni
Afisa Usalama na Mazingira kutoka shirika hilo Paul Thobias.
Banda
la Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi zake kama linavyoonekana
pichani kwenye kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam
International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa
Habari, Mhandisi Yisambi Shiwa (kushoto) na Mkaguzi wa Madini
Mwandamizi Jeremiah Hango (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kuwahudumia
wateja katika Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam
International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni