Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill
and Melinda Gates ya Marekani Bi. Melinda Gates akiongea na wadau
mbalimbali na kulipongeza shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa
kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo lengo kubwa ni
kuwawezesha wakulima wadogo wadogo wanawake kufanikiwa katika Kilimo
cha chakula na umiliki wa ardhi.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania
Jane Foster akitoa neno la utangulizi wakati wa sherehe hiyo.
Waziri wa Afya,Jinsia,Wazee na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu akilipongeza Shirika la Kimataifa la Oxfam
Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo
linaonesha changamoto za wazalishaji wa chakula wadogo ikiwemo
umiliki wa ardhi.
Dkt. Eve Marie akizungumza
kwa kina ni jinsi gani Serikali na Sekta binafsi zinaweza kuwekeza
katika wakulima wadogo wadogo hasa wanawake ili kuongeza
uzalishaji wa Chakula.
Muwezeshaji kutoka Forum CC Faizal
Issa akielezea namna wakulima ambavyo wanaweza kukabiliana na
mabadiliko ya Tabianchi ambayo kwa sasa yanaathiri kwa kiasi kikubwa
katika uzalishaji katika kilimo.
Mwanamuziki maarufu wa Muziki wa
kizazi kipya Bongo Fleva Mwasiti akitumbuiza wakati wa Sherehe hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni