Dr
Adelhelm James Meru akimkabidhi Flaviana Matata barua ya kuchaguliwa
kwake huku kaimu Mkurugenzi Devota Mdachi akishuhudia, katika ofisi za
wizara hiyo
Mwanamitindo wa Kimataifa anaefanyia
kazi zake za nchini Marekani Flaviana Matata amechagulia na Wizara ya
Maliasili kuwa Balozi wa Hiyari 'Good Will Ambassador' kwa kipindi cha
miaka mitatu kwa dhumuni la kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania
ndani na nje ya nchi.
Flaviana ambaye juzi alikuwa mmoja kati
ya shuhuda wa kushuhudia wizara ya maliasili na utalii wakizindua rasmi
tangazo litakalokuwa linatangaza vivutio vya Tanzania nje ya anchi
alitawazwa leo hii na katibu mkuu Dr Adelhelm James Meru aliyemkabidhi
kwa niaba ya Waziri , Mheshimiwa Lazaro Nyalandu huku Kaimu Mkurugenzi
Madam Devota Mdachi akishuhudia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni