Baraza la Taifa la Kudhibiti Ukimwi
nchini Kenya (NACC) limesema vijana 435,225 wenye umri wa kuanzia
miaka 10 hadi 19 wanamaambukizi ya Ukimwi, huku wengine 119,899
wakiwa na virusi vya ugonjwa huo lakini bado hawajatambuliwa.
Kwa mujibu wa baraza hilo kutokana
na idadi hiyo ya maambukizi ya Ukimwi, vijana 7,500 walifariki dunia
kwa ugonjwa huo mwaka jana nchini Kenya kutokana na kucheleweshewa
matibabu pamoja na kunyanyapaliwa mno.
Ripoti ya NACC inaonyesha kuwa
kaunti ya Nairobi inaongoza kwa kuwa na vijana 49,904 wenye kuishi na
maambukizi ya Ukimwi, Homa bay ya pili vijana 46,530 ikifuatiwa na
Kisumu ikiwa na vijana 37,110 walioathirika na Ukimwi, Siaya vijana
33,810 huku Marsabit ikiwa na vijana 450, Tana River 360 na Wajiri
ya mwisho ikiwa na vijana 150 waathirika wa Ukimwi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni