Karibu shule zote za umma nchini
Kenya, zinatarajiwa kufungwa hii leo kutokana na mgomo wa wiki tatu
wa walimu pamoja na ukosefu wa fedha za kuziendesha shule na kuwa
mzigo kwa uongozi wa shule.
Katika mahojiano na wakuu wa shule
za umma Kenya, yaliyofanywa na gazeti moja la nchini humo imebainika
hata shule zinazotaka kuendelea kuwepo wanafunzi shuleni zinakabiliwa
na ugumu kutokana na kukosa fedha za uendeshaji.
Wakati huo huo muda uliotolewa na
Tume ya Huduma za Walimu (TSC) kwa walimu kurejea kazini la sivyo
wataondolewa katika orodha ya malipo ya mshahara ya mwezi huu unaisha
leo, kwa mujibu wa agizo hilo lililotolewa wiki iliyopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni