Mmiliki na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Black Sensation, Lilliane Masuka (katikati),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi, kuhusu Tamasha la Fahari ya Mwafrika litakalofanyika viwanja
vya Club ya Escape One, Oktoba 3, 2015 Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni hiyo, Gabriel Manyaga na
Mkurugenzi wa Ubunifu wa kampuni hiyo, Charlotte Mwaigwisya.
Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa Kampuni ya Black Sensation, Gabriel Manyaga (kushoto),
akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mmiliki na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo, Lilliane Masuka.
Mkurugenzi wa Ubunifu wa kampuni hiyo, Charlotte Mwaigwisya akitoa ufafanuzi kwa waaandishi wa habari kuhusu tamasha hilo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Black Sensation inatarajia kufanya tamasha lenye kutangaza utamaduni
wa Mwafrika Oktoba 3 mwaka huu katika Club ya Escape One iliyopo
Mikocheni Jijini Dar es Salaam ambalo linatambulika kama 'Fahari ya
Mwafrika'.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mmiliki na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Liliane Masuka alisema tamasha
hilo ni la muhimu katika kuutangaza utamaduni wetu.
Masuka
alisema tamasha hilo linatarajiwa kuonyesha vitu mbalimbali vya asili
ya mwafrika na tamaduni zake litakuwa la aina yake kutokana na
maandalizi pamoja na washiriki.
Mkurugenzi
huyo alisema tamasha hilo litakuwa na lengo lake likiwa ni kuhamasisha
utamaduni na kubadilishana kimawazo pamoja na kufanya maonesha ta
tamaduni mbalimbali.
"Oktoba
3 mwaka huu tutakuwa na tamasha ambalo litatambulika kwa jina la
'Fahari ya Mwafrika' na tunatarajia kutakuwepo na vikundi mbalimbali
ambavyo vitaonesha utamaduni wetu," alisema.
Masuka
alisema katika tamasha hilo kutakuwepo na muziki wa dansi, vichekesho,
maigizo, ngoma na vitu mbalimbali ambavyo kwa pamoja vinatangaza
utamaduni wa Tanzania.
Alisema
pia kutakuwa na vikundi mbalimbali kutoka shule za Sekondari,
wanamitindo na wabunifu wa ndani ambao wataonesha vitu vyenye kuakisi
utamaduni wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa kampuni hiyo, Gabriel Manyaga alisema pamoja na kuanda
tamasha hilo pia wanatarajia kutoa tuzo za Fahari ya Afrika kwa watu
ambao wataonesha kuudumisha uafrika kupitia tamasha hilo kubwa na la
aina yake.
Alisema
tuzo zitatolewa kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali ambavyo kwa
pamoja vitazingatia sifa husika na sio kuchaguana kishabiki kama tuzo
zingine zinazotolewa.
Manyaga
alisema wao kama Black Sensation wanaamini kuwa wataweza kukuza na
kuibua vipaji vya wasanii wa hapa nchini ambao wameshindwa kuonekana na
kutambulika kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wao.
Mkurugenzi
wa Ubunifu wa Kampuni hiyo, Charlotte Mwaigwisya alisema kampuni hiyo
ilibuni tamasha hilo ili kutoa fursa ya kuutangaza utamaduni wetu ambao
kwa kiasi kikubwa umeanza kusahulika kutoka na sababu mbalimbali ikiwemo
kupungua kwa kasi ya kuutangaza.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni