Kamishna Msaidizi wa
Madini, Kanda ya Kati – Magharibi, Humphrey Mmbando akitoa ufafanuzi wa baadhi
ya masuala muhimu yaliyojitokeza wakati wa semina kwa wachimbaji wadogo wa
madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya
mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP). Semina hiyo
imefanyika leo mjini Shinyanga na ni mwendelezo wa Mafunzo yanayotolewa nchi
nzima kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchini. Wengine
pichani (mstari wa mbele) ni baadhi ya Maofisa kutoka Ofisi ya Madini –
Shinyanga.
Baadhi ya akina mama
ambao ni wachimbaji wadogo wa madini mkoani Shinyanga wakiwa katika semina
kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao
(Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP). Kutoka Kushoto ni Amina
Mtoro, Hafsa Issa, Halima Mohamed, Khadija Salum na Nusura Juma. Semina hiyo
imefanyika leo mjini Shinyanga na ni mwendelezo wa Mafunzo yanayotolewa na
Wizara ya Nishati na Madini kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za
madini nchi nzima.
Mtaalamu kutoka Kitengo
cha Leseni cha Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Nuru Shabani, akitoa
ufafanuzi kuhusu utaratibu wa utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao wakati akiwasilisha
mada kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa
njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP) kwa wachimbaji
madini wadogo, wakati wa Semina maalumu iliyofanyika leo Septemba 9, 2015 mjini
Shinyanga.
Mtaalamu kutoka
Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Juma Masoud akijibu baadhi ya
maswali yaliyoulizwa wakati wa Semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu
mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online
Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP). Semina hiyo imefanyika leo
Septemba 9, 2015 mjini Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa na
Wizara husika kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchini
kote.
Baadhi ya Vijana
ambao ni wamiliki wa leseni za madini mkoani Shinyanga wakiwa katika Semina
kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya
mtandao (Online Mining cadaster Transactional Portal – OMCTP) yanayotolewa na
Wizara ya Nishati na Madini nchi nzima. Kutoka Kushoto ni Juma Swalehe, Steven
Ngonyani, Salum Abdillah na Meshack Daniel. Mafunzo hayo kwa mkoa wa Shinyanga,
yamefanyika leo Septemba 9, 2015.
Mtaalamu kutoka
Wizara ya Nishati na Madini, Erick Mkoma, akisaini Kitabu cha Wageni katika
Ofisi ya Madini Kanda ya kati Magharibi iliyoko mjini Shinyanga. Wengine
pichani ni Juma Masoud (katikati) na Mhandisi Nuru Shabani (Kulia). Wataalam
hawa leo Septemba 9, 2015 wametoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa
leseni za madini mkoani Shinyanga kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za
utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandano (Online Mining Cadastre
Transactional Portal – OMCTP).
Na
Veronica Simba – Shinyanga
Zoezi la utoaji
semina kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchini
linaloendeshwa na wizara ya nishati na madini leo limefanyika mjini Shinyanga
ambapo wachimbaji zaidi ya 60 wamepatiwa mafunzo hayo.
Akifungua Semina hiyo
mjini Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Magharibi, Humphrey
Mmbando amewataka washiriki kuhakikisha wanaufahamu mfumo mpya wa utoaji leseni
za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal –
OMCTP) kwani ni wale tu watakaosajiliwa kwenye mfumo husika ndiyo
watakaotambuliwa kisheria na kupata haki zote za msingi.
Wizara ya Nishati na
Madini ilizindua mfumo wa kutoa huduma za leseni kwa njia ya mtandao mapema
mwezi Juni mwaka huu mjini Dodoma ili kutoa huduma za haraka, kuongeza uwazi na kumuwezesha mteja kusimamia leseni
zake mwenyewe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni