Mwenyekiti
 wa National Governance Internet Forum ambaye pia ni Rais wa Klabu za 
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya akiwakaribisha 
wadau wa mitandao na watumiaji wa intaneti kwenye jukwaa hilo kabla ya 
kumkaribisha mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA kufungua rasmi jukwaa
 hilo.. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tanzania Education and Research 
Network (TERNET), Amos Nungu na Kushoto ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, 
Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni 
(UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akifuatiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi 
Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Sunday Richard. (Picha 
zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Na Mwandishi Mwetu
SHIRIKA
 la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO), 
limewaomba wadau wa habari hasa wa matumizi ya intaneti kuzingatia 
maadili na usiri katika kazi zao ili kutovunja sheria zilizowekwa na 
mamlaka husika likiwemo suala la sheria ya mtandao iliyopitishwa hivi 
karibuni nchini Tanzania.
Hayo
 yameelezwa na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika 
la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin 
Yusuph aliyekuwa akimwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues 
katika Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya mtandao (NIGF), 
lililofanyika mwishoni mwa wiki na kuandaliwa na Umoja wa Klabu za 
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
UNESCO
  inaamini masuala ya usiri katika mitandao ni  njia bora zaidi za 
kuepukana na suala la  mmomonyoko wa maadili na usio zingatia taaluma.
Ambapo
 amebainisha kuwa, takribani Asilimia 84 ya  Mataifa  duniani wamegundua
 hawana  sheria madhubuti ya kulinda uhuru wa usiri kwa wananchi kupitia
 mitandao hivyo ni muhimu kuzingatia taaluma na maadili kwenye matumizi 
ya intaneti  hasa kwa kipindi hichi.
“UNESCO
 inaamini mambo muhimu ya kuzingatia juu ya matumizi ya mitandao ikiwemo
 kuwa na Uwazi, Upatikanaji na Ushirikishi. Kwa hayo machache,  mjadala 
huu wa matumizi ya mtandao unaweza kufanikiwa na sie tunapenda kuungana 
na nyinyi katika kushirikiana katika suala hili” alieleza Ofisa Miradi 
ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, 
Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Mwakilishi
 wa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Sunday 
Richard akifungua rasmi Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya 
mtandao (NIGF) lililoandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari 
Tanzania (UTPC) na kufanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano
 COSTECH jijini Dar. 
Kushoto
 ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la 
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph
 aliyemwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO na kulia Mwenyekiti wa National 
Governance Internet Forum, Kenneth Simbaya.
Aidha,
  katika mkutano huo, imeelezwa kuwa, matumizi  makubwa ya mtandao wa 
kompyuta (intaneti) yatasaidia ongezeko la pato la taifa (GDP).
Kauli
 hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya jukwaa la 
mtandao wa intaneti (IGF) Kenneth Simbaya wakati wa jukwaa hilo ambapo 
amebainisha kuwa, katika matumizi yake ni muhimu sana kujadili 
kutengeneza kesho wanayoitaka watanzania katika matumizi ya mtandao.
Ameeleza
 chombo cha IGF  kimelenga kuangalia maendeleo ya mtandao nchini usalama
 wake na matumizi ya mtandao yanayoelenga kubadilisha maisha ya 
watanzania kwani chombo hicho nchini Tanzania kimeundwa kutokana na  
mkutano wa kimataifa wa jamii ya wanahabari (WSIS)  waliotaka kuwepo na 
jukwaa kuangalia matumizi ya matandao kutokana na kuongeza kwa haja ya 
matumizi.
Simbaya
 amesema Majukwaa hayo yanatakiwa kuzungumza kuhusu sera  kwa lengo la 
kuangalia uendelevu wake , usalama, ukuaji wa mtandao wenyewe na 
menejimenti yake.
Kwa
 upande wake Mtaalamu kutoka TCRA Dk. Emmanuel Manasseh  akithibitisha 
umuhimu wa mtandao katika maisha ya sasa na yajayo,  alielza kwamba kama
 kutakuwepo na ongezeko la watumiaji angalau kwa asilimia 10 pato la 
taifa litaongezeka kwa asilimia 1.4. zaidi.
Ambapo
 anaendelea kubainisha kuwa, kwa sasa idadi ya watumiaji wa mtandao 
wameongezeka kufikia asilimia 11 na kwamba lugha ya mtandao kwa sasa 
inaathiri watu mbalimbali kwa namna njema na namna mbaya.
Jukwaa
 hilo pamoja na kuzungumza kuhusu uendelevu wake pia ulizungumzia  
sheria , kanuni na taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa katika matumizi na 
utawala wa intaneti ili kuzifanya zitumike kwa makusudio mema zaidi.
Naye
 mtaalamu wa masuala ya mtandao wa intaneti, Maxence Melo kutoka Jamii 
Forum amesema kwamba mpaka sasa anaona kwamba matumizi ya mtandao 
Tanzania bado salama ingawa juhudi lazima ziendelee kufanyika 
kuhakikisha kwamba hali ya usalama inaendelea kuwapo.
Ofisa
 Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la 
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph 
aliyemwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO akitoa salamu za shirika la UNESCO 
wakati  wa mkutano wa  Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya 
mtandao (NIGF) ulioandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari 
Tanzania (UTPC).
Katibu
 Mtendaji wa Tanzania Education and Research Network (TERNET), Amos 
Nungu akitoa salamu za TERNET kwa wadau waliohudhuria jukwaa hilo.
Mtaalamu
 kutoka TCRA Dk. Emmanuel Manasseh akiwasilisha mada iliyoelezea umuhimu
 wa mtandao katika maisha ya sasa na yajayo wakati wa jukwaa hilo.
Pichani
 juu na chini ni sehemu ya washiriki waliohudhuria jukwaa hilo 
wakifuatilia "presentation" iliyokuwa ikitolewa na Mtaalamu kutoka TCRA 
Dk. Emmanuel Manasseh (hayupo pichani).
Ofisa
 Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la 
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph kwa mtaalamu
 kutoka TCRA (hayupo pichani) kama wana mipango gani kuhakikisha kuwa 
kutakuwepo na masafa ya kutosha kwa miaka mingi ijayo kwaajili ya 
wananchi wa vijijini na wale wasio na uwezo.
Picha ya pamoja.
Maxence
 Melo kutoka Jamii Forum akizungumza na waandishi wa habari wakati wa 
jukwaa lililowakutanisha  kwa pamoja wadau wa masuala ya mitandao ya 
intaneti.
Maxence
 Melo kutoka Jamii Forum (katikati) akipata picha ya pamoja na wajumbe 
wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Fredy Njeje wa Blog za Mikoa (kulia)
 na Mr. Verbs.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni