RAIS Jakaya Kikwete jana amewatunuku kamisheni maafisa wa jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ) 166, wa kundi namba 56/14, katika Chuo cha
Mafunzo ya Kijeshi kilichopo Monduli, Mkoani Arusha.
Miongoni mwa waliotunikiwa nishani hizo ni wanawake 21 na wanaume 145
ambao kwa pamoja walikula kiapo cha utii na wanafunzi waliofanya
vizuri katika mafunzo hayo aliwatunuku zawadi.
Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mafunzo hayo na
kutunukiwa zawadi ni Martina Simba, Nuru Mhama, Sham Mbegu na
mshindi wa jumla ni Anthony Shija.
Hii ni Kamisheni ya mwisho kabla ya kuondoka katika kiti hicho, Rais
Jakaya Kikwete kuitoa chuoni hapo, ambapo katika uongozi wake
alitunuku wanafunzi 2,707 ambao ni wanaume na wanawake ni 302 na
wanafunzi wanajeshi waliotoka katika nchi mbalimbali walikuwa ni 594
kati yao wanawake ni kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Baada ya kutunuku kamisheni hizo, pia aliangalia vikundi mbalimbali
vya sanaa, ambavyo aliandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga.
Pia halfa hiyo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda,
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ,Mawaziri Wakuu wa Vyuo kutoka
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na wananchi
mbalimbali.
Rais pia alipewa zawadi mbalimbali kwa kuthamini mchango wake, chuoni
hapo yeye pamoja na Mkewe ,Mama Salma Kikwete.
Mwisho.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni