Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Martin Loibooki akiongea na wanakijiji wa
Olosinoni wanaoshiriki zoezi la kuzima moto unaonendelea kuwaka Mlima
Meru katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha jana.
Moto unaoendelea kuwaka Mlima Meru katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Moto
mkubwa umezuka mwishoni mwa wiki hii na kuunguza sehemu ya Mlima Meru
katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa
chanzo cha moto huo ni vitendo haramu vya urinaji wa asali ndani ya
msitu wa hifadhi hiyo.
Wananchi wapatao 200 kutoka vijiji jirani
vya Olosinoni na Kisimiri Juu wakishirikiana na TANAPA wamefanikiwa
kuudhibiti moto huo ili usiweze kuleta madhara makubwa kwa binadamu
hususan wageni wanaotembelea hifadhi kwa lengo la kupanda Mlima Meru.
Hadi
sasa hakuna wageni waliodhurika na moto huo na tahadhari zote
zimechukuliwa ili kudhibiti madhara zaidi kwa binadamu na shughuli za
utalii ndani ya hifadhi.
Shirika la Hifadhi za Taifa linaendelea
kuwatahadharisha wananchi juu ya vitendo vya kuingia ndani ya hifadhi
bila kibali kwa shughuli ambazo zinaweza kuwa chanzo cha kuzuka kwa
mioto hii ambayo husababisha uharibifu wa mazingira pamoja na kuharibu
vyanzo vya maji.
Aidha, katika kuhakikisha kuwa moto huo
unadhibitiwa kwa haraka, TANAPA imeongeza nguvu kazi ya wananchi
wakishirikiana na vyombo vingine vya dola ili kuweza kuudhibiti moto
huo.
Mwisho, taarifa kamili juu madhara yaliyosababishwa na moto
huo itatolewa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuzima moto na umma
utaendelea kupewa taarifa ya maendeleo ya zoezi la uzimaji wa moto kila
wakati.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
21.09.2015
dg@tanzaniaparks.com
www.tanzaniaparks.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni