SERIKALI YA CCM KUTOA MILIONI 150 KILA KATA DAR ES SALAAM KWA WAJASIRIAMALI


Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza kwenye Viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es Salaam.[/caption]

SERIKALI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imepanga kutoa shilingi milioni 150 kwa kila Kata ya Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali kimikopo ili kukuza biashara zao. Kauli hiyo imetolewa na Mgombea mwenza wa CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Mbezi Centre jijini Dar es Salaam.

Alisema ili kuboresha huduma za afya Jimbo la Kibamba Serikali imedhamiria kujenga hospitali kubwa itakayofanya kazi saa 24 pamoja na kuboresha huduma nzima za afya katika hospitali hiyo wakiwemo wataalam.

Aliongeza kuwa Serikali kupitia mradi mkubwa wa maji safi na salama imepanga kuongeza huduma za usambazazi maji kwenye eneo la Kibamba na kiujumla mradi mzima utakapokamili hali ya upatikanaji maji itapanga kutoka asilimia 65 ya watu hivi sasa hadi kufikia asilimia 95 jambo ambalo litamaliza kero kabisa ya maji Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu kwenye uwanja wa Mbezi Centre Kata ya Mbezi jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo Serikali ya CCM imepanga kuyapima maeneo ya viwanja na kuyakabidhi kwa wananchi jimboni humo ili kuwawezesha wamiliki kuyatumia kama dhamana pamoja na kuwalipa fidia wananchi 8,365 wa Mloganzila ili kupisha uendelezaji wa eneo lililoitajika kwa maendeleo.

Mgombea mwenza alifanya mikutano yake ya kunadi ilani ya CCM katika Jimbo la Kinondoni maeneo ya Mbezi, Mburahati, Mwananyamala na Msasani (Namanga) jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu kwenye Viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es Salaam
Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akiwanadi wagombea udiwani wa Jimbo la Kawe kwenye mkutano wa kampeni ulofanyika kwenye Viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es Salaam.

Meya wa Kinondoni, Yusuf Mwenda akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es Salaam.

Hawa Ng'umbi akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Jimbo la Kawe kwenye mkutano wa kampeni ulofanyika kwenye Viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es Salaam.

                                                               *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni