Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Uchaguzi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Uchaguzi. Onyesha machapisho yote

TUPIGE KURA, TUPOKEE MATOKEO KWA AMANI NA UTULIVU, KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI

JUMAPILI ya Oktoba 25, 2015, Tanzania inafanya Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge pamoja na kumpata Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uchaguzi ni nini? Zipo tafsiri mbalimbali lakini mojawapo na iliyo wazi ni kwamba, hii ni njia ya kidemokrasia inayotumiwa na watu katika kuchagua viongozi wa kuwaongoza kwa kipindi fulani kwa mujibu wa Katiba au utaratibu waliojiwekea wenyewe.


Huu ni Uchaguzi Mkuu wa Tano kufanyika tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza tena mwaka 1992, lakini ni wa 11 tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964.

Uchaguzi wa mwaka huu una umuhimu wa kipekee kwa sababu kadha wa kadha, mojawapo ikiwa umri wa miaka 23 tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza.

Huu ni umri mkubwa, na kwa hakika vijana wengi waliojitokeza kujiandikisha safari hii ni wenye umri wa kati ya miaka 18-35, ikimaanisha kwamba wengi wao walizaliwa kuanzia mwaka 1992. Hawa wanatengeneza asilimia 57 ya wapigakura wote.

Umuhimu mwingine ni kwamba, kulinganisha na uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, safari hii demokrasia imekua na kupanuka kiasi cha kushuhudia wapigakura 22.75 milioni, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini tangu tupate Uhuru.

Kwa upande mwingine, hamasa imeongezeka, upinzani umeimarika zaidi na uhuru wa habari umepanuka ukiwamo ukuaji wa sekta ya habari na mawasiliano, hususan mitandao ya kijamii.

Haya yote yanatokea kutokana na kuwapo kwa amani na utulivu, sifa ambazo zimeendelea kuitambulisha vyema Tanzania hata katika jumuiya za kimataifa.

Uchaguzi Mkuu ni gharama kubwa kifedha, rasilimali watu na muda, na kama mambo yatakwenda mrama maana yake nchi itakuwa imeingia hasara kwa kupoteza fedha, lakini pia itaingia kwenye machafuko ambayo yatatowesha amani iliyodumu kwa miaka mingi.



Madhara ya machafuko au vita – kama tulivyoshuhudia kwa majirani zetu Rwanda na Kenya ni vifo, ulemavu wa kudumu, kutengana na familia, ukimbizi na kuvurugika kwa uchumi, jamii na siasa kwa ujumla.

Kwa miaka yote tangu Uhuru, licha ya uchanga na umaskini kama taifa, Watanzania hatujazoea maisha ya vurugu na machafuko na ndiyo maana tuna wajibu wa kuhakikisha uchaguzi huu unapita salama.

Wajibu wa kulinda amani ya nchi yetu ni wa kila Mtanzania bila kujali rangi, dini, kabila ama nafasi yake katika jamii.
Tunaposema hivyo tunamaanisha kwamba, vyombo vya dola vinapaswa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha Watanzania wanapiga kura kwa amani kuchagua viongozi wao kwa utaratibu waliojiwekea.

Kimsingi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ndio wasimamizi wa chaguzi zote, hivyo wana dhamana kubwa kuhakikisha kila aliyejiandikisha na kujitokeza siku hiyo anatumia haki yake ya kikatiba kupiga kura bila kubughudhiwa.

Ili kuondoa utata huo, NEC pia inapaswa kuhakikisha kunakuwa na uwazi kuanzia hatua ya kupiga kura mpaka wakati wa kutangaza matokeo, ambayo pia yanatakiwa kutolewa kwa wakati ili kuondoa mashaka miongoni mwa wagombea na wananchi kwa ujumla.

Wanasiasa, hususan wagombea ama wapambe wao, wanapaswa kutoa kauli za kuhamasisha amani na utulivu kwa siku hizi chache zilizosalia kuelekea uchaguzi mkuu, siku ya uchaguzi na baada ya kutangazwa kwa matokeo.

Wanasiasa wanaaminika kwa wananchi, kwa hiyo kauli yoyote watakayoitoa ama inaweza kujenga au kubomoa amani iliyopo, hivyo kuondoa utulivu na kuisambaratisha Tanzania ya sasa iliyotukuka ulimwenguni kote kama kisiwa cha amani na utulivu.

Vyombo vya habari navyo vina wajibu mkubwa zaidi kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa usalama na amani na hata baada ya matokeo kutangazwa viendelee kudumisha amani hiyo.

Hilo litawezekana tu iwapo vyombo vya habari vitaandika au kutangaza habari kwa kufuata sheria za nchi, miiko na maadili ya taaluma na fani ya uandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kutoegemea upande wowote, kuepuka lugha za uchochezi na ushabiki wa kisiasa, kabla na wakati wa kutangaza matokeo.

Kutokana na umuhimu huo, sisi wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania (Bloggers) tumejadiliana na kukubaliana kwa pamoja kuhusu hatma na mustakabali wa taifa letu kuhakikisha amani na utulivu vinadumishwa wakati na baada ya uchaguzi huu wa kidemokrasia na kwa kauli moja tumetoa msimamo wetu kuhusu amani ya nchi hii.

Kwa ujumla, hakuna anayeweza kujisifu kuwa ana uhalali zaidi wa taifa hili kuliko mwingine, taifa hili ni letu sote, hivyo wajibu wa kulinda na kudumisha amani na usalama wa nchi ni wa kila mmoja.

Tunaomba Watanzania wote wenye sifa wajitokeze kupiga kura kwa amani na utulivu, wasubiri matokeo kwa amani na utulivu, wapokee matokeo kwa amani na utulivu, maisha yaendelee kwa amani na utulivu, tusonge mbele kwa amani na utulivu huku tukijua kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi, na hilo ndilo muhimu zaidi.

                                                                                         MUNGU IBARIKI TANZANIA!

MAMA SAMIA NA DK. SHEIN WAFUNGA KAZI MKUTAO WA KUFUNGA KAMPENI ZA CCM ZANZIBAR

Maelfu ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM, uliofanyika leo kwenye Viwanja hivyo mjini Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohammed Shein akisalimiana na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu hassan baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.
Mgombea wa Urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein akimsalimia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar leo. Wengine ni Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Waziri Kiongozi Mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha
Mgombea Mwenza Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo katika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar

LOWASSA AHUTUBIA RUAHA

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiongea na wananchi wa Ruaha katika viwanja vya Tem K2 Ruaha leo Ijumaa 23/10/2015
Mgombea ubunge wa jimbo la Mikumi Joseph Haule akimueleza matatizo ya Mikumi Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa pamoja na kuzungumza na wananchi waliofika katika viwanja vya Tem k2, leo Ijumaa 23 Oktoba 2015
                                                            Wananchi wakishangilia katika mkutano huo
Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa pamoja na Mhe. Fredrick Sumaye wakiwasili katika viwanja vya Tem K2 Ruaha, leo Ijumaa 23/10/2015. Kwa hisani ya ZanziNews

MTOTO HATUMWI DUKANI LEO . NI KATIKA UFUNGAJI WA KAMPENI ZA CCM JIJINI MWANZA.


Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Pichani) amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya shughuli ya kufunga kampeni za Uchaguzi Mkuu kitaifa kwa upande wa Chama hicho inayotarajiwa kufanyika hii leo katika Uwanja wa CCM Kirumba yamekamilika.

                                                                                                   Na:George Binagi-GB 

Pazzo kubwa itafungwa nje ya uwanja huo kwa ajili ya wale watakaokosa nafasi ya kuingia uwanjani kwa kuwa shughuli hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na Maeneo jirani.

Mbali na Mgombea Urais wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli kuwepo katika mkutano huo, pia Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaemaliza muda wake Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa miongoni mwa viongozi watakaohudhuria katika Mkutano huo wa Ufungaji wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa upande wa CCM.

Wakati Watanzania wakitarajia kushiriki zoezi la Uchaguzi Mkuu siku ya kesho jumapili ya Octoba 25, Chama cha Mapinduzi CCM kimejihakikishia ushindi mnono katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia ngazi ya udiwani, Ubunge na Urais.

Shamra shamra kwa makada wa CCM zimepamba moto katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza katika kuelekea kwenye ufungaji wa kampeni za chama hicho kitaifa unaofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba.

MGOMBEA MWENZA WA CHADEMA JUMA DUNI HAJI AHUTUBIA MKUTANO MJINI DODOMA


 Mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji akihutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe mkoani Dodoma. 
Wakazi wa Dodoma wakimsikiliza mgombea mwenza wa urais Chadema anayeungwa mkono na Ukawa akizungumza katika mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe.
 Waendesha Bodaboda wakimsindikiza mgombea mwenza wa urais, Juma Duni Haji wakati alipomaliza kuhutubia wakazi wa Dodoma katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe.
Kikundi cha ngoma cha Moto Kali kutoka Ibiwa wakicheza ngoma ya kumkaribisha mgombea mwenza wa urais wa Chadma Juma Duni Haji kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Kongogo mkoani Dodoma.
 Mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji akimnadi kwa wananchi wa Bahi mgombea wa Ubunge Jimbo la Bahi, Mathias Lyamundu kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Kongogo mkoani Dodoma.
  Mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji akimnadi mgombea wa Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Benson Kigaila kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe mkoani Dodoma.
Aliyekuwa mbunge wa Mkanyageni Zanzibar, Habibu Mohamed Mnyaa akihutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe mkoani Dodoma.
 Wakazi wa mjini Dodoma wakifuatilia mkutano huo.
 Wazee katika mkutano.

Yusufu Makamba Amla Nyama Kingunge; “Ukitaka Kumtukana Baba Yako Mshukuru Kwanza”

atika mkutano mkuu wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa Tabora mjini ndg Emmanuel Mwakasaka, Katibu mkuu mstaafu wa CCM Taifa mzee Yusufu Makambakama mgeni rasmi azungumzia mengi ikiwa kumnadi Mgombea Urais, mgombea Ubunge na madiwani wote wa CCM, pia azungumzia suala la Kingunge na Lowassa katika mkutano uliofanyika kituo cha zamani cha mabasi mkoani Tabora. Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (27)
Yusufu Makamba, mkongwe wa siasa nchini akiongea na wananchi wa Tabora mjini.
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (28)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (29)
Yusufu Makamba akizungumzia upotofu mkubwa dhidi ya Kingunge aliyedai kuwa CCM imekosa pumzi baada ya kuihama CCM huku yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa miongoni mwa waandishi mbalimbali wa vitabu vya mielekeo mbalimbali ya chama na waandamizi wa kubwa wa CCM. “…aliingia CCM akiwa na meno na ametoka CCM akiwa hana meno… yeye ndiye asiye na pumzi CCM bado iko imara na ina pumzi ya kutosha…” Alisema Makamba
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (30)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (36)
Makamba (Kushoto) akimtaka Rage (Mbunge anayeachia madaraka) kuzungumza machache na wananchi.
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (37)
Mwakasaka (Kushoto-Mgombea Ubunge) na Rage. Wawili hawa waliokuwa mahasimu katika kusaka kura za maoni za kupewa ridhaa ya kugombea ubunge mjini Tabora wakiwa pamoja jukwaani na kuonesha kwamba wako pamoja huku ndg Aden Rage akimuombea kura za ushindi ndg Mwakasaka.
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (33)
Yusufu Makamba akimuonya mgombea ubunge Ndg Mwakasaka kutoleta lelemama kwa wananchi wenye ridhaa ya kumpigia kura za ubunge
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (18)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (19)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (20)
Kushoto: Munde Tambwe (Mbunge mtarajiwa wa Viti maalum mkoani Tabora) na mbunge anayemaliza muda wake Ndg Aden Rage wakifuatilia jambo.
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (25)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (39)
Ndg. Mwakasaka akiomba kura kwa wananchi waliokusanyika kwa wingi kusikiliza sera za mgombea wao katika uzinduzi huo uliofanyika katika kituo cha zamani cha mabasi Tabora.
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (38)
Mwakasaka akisisitiza jambo kwa wananchi.
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (40)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (35)
Kwa nyakati tofauti, mzee Yusufu Makamba katika picha ya juu na chini alitumia muda wake kuwanadi wagombe udiwani wa jimbo la Tabora mjini
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (34)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (32)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (26)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (22)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (41)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (17)
Mwakasaka_ccm_tabora-2015 (23)
******
Mzee Yusufu Makamba (Katibu mkuu mstaafu wa CCM Taifa) akiwa Unyamwezini mkoani Tabora jana kama mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa uzinduzi wa kampeni za kisiasa za mgombea wa ubunge jimbo la Tabora mjini ndg Emmanuel Mwakasaka kwa tiketi ya CCM ulifanikiwa hasa kwa kuhakikisha anamla nyama zote mzee Kingunge kufuatia kujing’atua katika chama cha CCM alichokitumikia kwa miaka mingi sana.

Mzee Yusufu Makamba kama mgeni rasmi wa mkutano huo alisisitiza kuwa wananchi wahakikishe wanawapa kura zao wagombea wa CCM ili serikali ijayo iendeleze mikakati iliyopo na ijayo katika kuijenga nchi ya Tanzania na si Vinginevyo.

LOWASSA ATIKISA MUSOMA,AENDELEA KUSABABISHA MAFURIKO

 
 
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vicent Nyerere, wakiwasili kwenye Uwanja wa Mkendo, Jimbo la Musoma Mjini, Mkoani Mara .
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vicent Nyerere, akihutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkendo, Jimbo la Musoma Mjini, Mkoani Mara .
 
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Musoma waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Mkendo, Jimbo la Musoma Mjini, Mkoani Mara.
 
 
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia 
mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Musoma 
katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa 
Mkendo, Jimbo la Musoma Mjini, Mkoani Mara  Oktoba 11, 2015.