Yusufu Makamba, mkongwe wa siasa nchini akiongea na wananchi wa Tabora mjini.
Yusufu Makamba akizungumzia upotofu
mkubwa dhidi ya Kingunge aliyedai kuwa CCM imekosa pumzi baada ya
kuihama CCM huku yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa miongoni mwa waandishi
mbalimbali wa vitabu vya mielekeo mbalimbali ya chama na waandamizi wa
kubwa wa CCM. “…aliingia CCM akiwa na meno na ametoka CCM akiwa hana
meno… yeye ndiye asiye na pumzi CCM bado iko imara na ina pumzi ya
kutosha…” Alisema Makamba
Makamba (Kushoto) akimtaka Rage (Mbunge anayeachia madaraka) kuzungumza machache na wananchi.
Mwakasaka (Kushoto-Mgombea Ubunge) na
Rage. Wawili hawa waliokuwa mahasimu katika kusaka kura za maoni za
kupewa ridhaa ya kugombea ubunge mjini Tabora wakiwa pamoja jukwaani na
kuonesha kwamba wako pamoja huku ndg Aden Rage akimuombea kura za
ushindi ndg Mwakasaka.
Yusufu Makamba akimuonya mgombea ubunge Ndg Mwakasaka kutoleta lelemama kwa wananchi wenye ridhaa ya kumpigia kura za ubunge
Kushoto: Munde Tambwe (Mbunge mtarajiwa
wa Viti maalum mkoani Tabora) na mbunge anayemaliza muda wake Ndg Aden
Rage wakifuatilia jambo.
Ndg. Mwakasaka akiomba kura kwa wananchi
waliokusanyika kwa wingi kusikiliza sera za mgombea wao katika uzinduzi
huo uliofanyika katika kituo cha zamani cha mabasi Tabora.
Mwakasaka akisisitiza jambo kwa wananchi.
Kwa nyakati tofauti, mzee Yusufu Makamba
katika picha ya juu na chini alitumia muda wake kuwanadi wagombe udiwani
wa jimbo la Tabora mjini
******
Mzee Yusufu Makamba (Katibu mkuu mstaafu
wa CCM Taifa) akiwa Unyamwezini mkoani Tabora jana kama mgeni rasmi
katika mkutano mkuu wa uzinduzi wa kampeni za kisiasa za mgombea wa
ubunge jimbo la Tabora mjini ndg Emmanuel Mwakasaka kwa tiketi ya CCM
ulifanikiwa hasa kwa kuhakikisha anamla nyama zote mzee Kingunge
kufuatia kujing’atua katika chama cha CCM alichokitumikia kwa miaka
mingi sana.
Mzee Yusufu Makamba kama mgeni rasmi wa
mkutano huo alisisitiza kuwa wananchi wahakikishe wanawapa kura zao
wagombea wa CCM ili serikali ijayo iendeleze mikakati iliyopo na ijayo
katika kuijenga nchi ya Tanzania na si Vinginevyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni