BENDI
ya Yamoto na Kalunde zinatarajiwa kutumbuiza wakati wa sherehe za Tuzo
za Wanamichezo Bora na Tuzo ya Heshima ya Rais Jakaya Kikwete leo
Jumatatu Oktoba 12, 2015.
Maandalizi
kuhusiana na tuzo hizo zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari
za Michezo nchini (TASWA) yamekamilika kwa kiasi kikubwa na baadhi ya
wanamichezo wanaotoka nje ya Dar es Salaam ambao ni miongoni mwa
watakaopewa tuzo wanatarajiwa kuwasili leo jioni tayari kwa shughuli
hiyo.
Tunaamini
uwepo wa Yamoto na Kalunde itakuwa burudani nzuri kwa watakaohudhuria
sherehe hizo, ambapo wachezaji 10 waliong’ara zaidi katika miaka 10 ya
Rais Kikwete wanatarajiwa kupewa tuzo.
Pia
TASWA itatoa Tuzo ya Heshima kwa Rais Kikwete pamoja na viongozi watano
wa michezo 10 waliofanya vizuri zaidi katika miaka hiyo 10 na pia
kutakuwa na tuzo kwa kampuni au taasisi zilizofanya vizuri michezoni kwa
muda huo.
Tukio
hilo ambalo pia litahudhuriwa na Rais Kikwete lina lengo pia la
kuwakutanisha wanamichezo na kumuaga Rais Kikwete anayemaliza muda wake
kikatiba baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 25,
mwaka huu.
Tunawaomba kutokana na ugeni mzito utakaokuwepo katika
shughuli hiyo, ni vyema wageni waalikwa wakajitahidi kujali muda kwa
kufika kwa wakati ili kuepuka usumbufu mwingine watakaoweza kuupata
utakaosababishwa na kuchelewa kuingia kwao ukumbini.
Wadhamini wa
shughuli hiyo itakayoanza saa 12 jioni kwa wageni waalikwa kuanza
kuwasili ukumbini ni GSM Foundation, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
(TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Kampuni ya Salim Said
Bakhressa (SSB) na Megatrade Investiment.
Tunawaomba kutokana na
ugeni mzito utakaokuwepo katika shughuli hiyo, ni vyema wageni waalikwa
wakajitahidi kujali muda kwa kufika kwa wakati ili kuepuka usumbufu
mwingine watakaoweza kuupata utakaosababishwa na kuchelewa kuingia kwao
ukumbini.
Ahsanteni,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA11/10/2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni