Wananchi wa jimbo la Arumeru Mashariki wakiwa katika mstaari kwa ajili ya kupiga kura hii leo
Baadhi ya wananchi wa jimbo la Arumeru mashariki wamepongeza tume ya uchaguzi kwa jinsi walivyofanya maandalizi ya siku hii ya kupiga kura jambo kuna changamoto chache zilizojitokeza.
Hayo wamebainisha leo wakati walipokuwa wakiongea mwandishi wa habari hizi kusema kuwa tume ya taifa ya uchaguzi kwa mwaka huu wamejitaidi kuboresha huduma zao kuanzia katika daftar I la kudumu la kupiga kura pamoja na jinsi ya wananchi wanavyopiga kura.
Mmoja wa mwananchi ambaye alikuwa akipiga kura katika kituo cha Ngateu kilichopo katika kata ya Kiranyi ndani ya jimbo la Arumeru Mashariki Pelaji Massae alisema kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni wakipee na utaweka historia kwa nchini na kwa mataifa kwa ujumla.
Alisema kuwa katika uchaguzi huu wananchi wengi wameamka mpaka sehemu za vijijini wametambua maana halisi ya siasa,wamejua faida za kupiga kura na kumchagua kiongozi atakae muongoza na atake mletea maendeleo.
Naye mwananchi mwingine wa kituo cha Sakina Lomayani Laizer alisema kuwa amefurahi kuona vijana wengi ,pamoja na wanaume wengi wamejitokeza kwa wingi kupiga kura na hii ni dalili inaonyesha kuwa wananchi wametambua jinsi ya kutumia haki yao ya msingi ,pamoja na faida ya kumchagua kiongozi wanaemtaka.
Alisema kuwa pia katika kipindi hichi swala la rushwa limepungua kwani wananchi wengi wamejua faida ya kuchagua kiongozi bora na kuchagua kiongozi bila ya kupewa rushwa ya aina yeyote.
“kweli Rushwa katika kipindi hichi haina nafasi na hajawahi kuonekana tangu kipindi cha kampeni kianze na watu wameelimika kupita kiasi” alisema Raimondi kibori
Naye Rehema bakari alisema kuwa anapenda kuwasihi jinsi walivyoweza kutulivu katika kipindi cha kampeni pamoja na leo katika kupiga kura ndio watulie ivyo ivyo katika kipindi cha kupokea matokeo ili inchi yetu iendelee kuwa katika histoa ya nchi yenye amani pamoja na utulivu.
Mwandishi huyu aliweza kushuhudia mamia ya watu wakijitokeza kupiga kura kwa utulivu huku maeneo mbalimbali ya mkoa huu yakiwa na utulivu tofauti na siku nyine ,sanjari na kushuhudia jeshi la polisi wakiendelea kulinda amani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni